Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda (kulia) akiwa na mshtakiwa mwenzake Saleh Mkadamu wakielekea kupanda basi la magereza baada ya hukumu ya kesi yao ya uchochezi kuahirishwa hadi Mei 9. Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 wanakabiriwa na makosa matano ya kula njama na kuingia kwa jinai katika uwanja namba 311/3/4 kitalu T uliopo Markaz Chang'ombe na wizi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya Shs milioni 59 mali ya kampuni ya Agritanza.
Saleh Mkadamu akipanda basi kuelekea mahabusu
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda akipanda basi la magereza.
Ulinzi mkali kila kona ya mahakama
Askari wakiimarisha ulinzi nje ya Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Msafara wa magari ya Polisi wakisindikiza gari la magereza lililomchukua Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda wakati wakielekea mahabusu baada ya hukumu ya kesi yao kuahirishwa leo hadi Mei 9.
Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa wamekusanyika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo wakati hukumu ya kesi yake ilipoahirishwa leo.Picha na Habari Mseto Blog
1 comment:
Allah mkubwa bwana wanacheza naye piga salaam keshi itakwisha ukiwa katika haki huwezi kuzulumiwa katu abadan na mwisho wa siku utaachiwa tu wanashazoea kuwabandikiza watu kesi mchwra mchwara.
Post a Comment