ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 18, 2013

Wabunge sita wa Chadema wasimamishwa kushiriki shughuli za bunge kwa siku 5.

Wabunge sita wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema akiwemo mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni wamesimamishwa Kushiriki katika shughuli za bunge kwa siku tano baada ya kutokea hali ya sintofahamu bungeni April 17,2013 wakati mkutano wa 11 ukiwa katika kikao chake cha nane ukiendelea,hali iliyomlazimu naibu spika wa bunge Job Ndugai kusitisha shughuli za bunge katika hali isiyo yakawaida

1 comment:

Anonymous said...

Machozi yamenidondoka nilipokuwa nasikiliza taarifa ya vurugu kubwa ya "waheshimiwa" bungeni!!! Kweli jamani Tanzania imefikia hapo? utulivu, amani na usikivu umepotea kabisaa!! Wabunge badala ya kutuliza fujo ninyi ndo mwaanzisha fujo,vurugu na kutumia lugha mbaya hadharani!! eeeh Mungu ibariki Tanzania.