ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 12, 2013

KUWATENGA WALEMAVU NI KINYUME NA MKATABA WA KIMATAIFA

SERIKALI ya Zanzibar imesema haona mpango wa kujenga vituo maalumu kwa ajili ya kuwatunza watu wenye ulemavu kwani kufanya hivyo ni kinyume na utekelezaji wa matakwa ya Mkataba wa kimataifa.

Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Alhabib Ferej, aliyasema hayo jana wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi (CUF) Saleh Nassor Juma, aliyetaka kujua kama serikali ina mpango wa kuanziha vituo vya kuwatunza watu wenye ulemavu.

Waziri Fatma, alisema kwa mujibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2006, ya Mkataba wa Kimataifa ya kulinda haki za watu wenye ulemavu inapinga uwepo wa vituo vya aina hiyo.

Kutokana na matakwa hayo ya sheria, serikali ya Zanzibar , haina mpango wa aina yoyote wa kuweka vituo hivyo, kwani kwa mujibu wa matakwa ya mkataba huo, unahitaji kuwepo kwa ushirikishwaji katika jamii.

Alisema sheria hiyo pia imekuwa inataka watu wa aina hiyo kuwa na misingi ya uhuru, kuwatambua, kufurahia maisha, kuwaondolea vizuizi vitavyowanyima kuishi vyema katika jamii.

Alisema serikali ya Zanzibar , inaalazimika kufuata sheria hiyo baada ya Tanzania kuiridhia Mkataba huo wa Kimaataifa wa haki Fursa za Watu Wenye Ulemavu ambao uliwekewa saini hiyo Mwezi Oktoba 2010.

Akijibu suala la mmoja wa Wawakilishi hao aliyetaka kujua michango iliyochangwa kupitia mfuko ulioanzishwa na Wizara hiyo imezitumiaje kuwasaidia walemavu, Waziri huyo, alisema hadi sasa fedha ambazo hadi sasa zimeweza kupatikana kuchangia mfuko huo hadi sasaa ni shilingi milioni 250 ambazo zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya kuwanunulia vifaa vya kuwasaidia.

Akitaja vifaa hivyo ni pamoja na fimbo kwa watu wasioona, visaidizi vya kuingeza kusikia, vifaa vya kusomea kwa mazigira maalum ya watu hao.

Hata, hivyo, Waziri huyo aliwataka Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Viongozi wengine ambao waliahidi kutoa mchango wao kwa ajili ya kusaidia mfuko huo, kutimiza ahadi zao kwani mfuko huo ni endelevu kwa mahitaji ya watu wenye ulemavu.

1 comment:

Anonymous said...

Jibu zuri ni kuwa serikali haina uwezo wa kujenga makazi ya walemavu au ujenzi huo siyo priority. Hakuna ushahidi unaothibitisha umoja wa mataifa kupinga ujenzi huo na mataifa yenye uwezo ambayo yapo nda ya baraza la usalama la umoja wa mataifa wmewajenge makazi walemavu.