Zanzibar. Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe imeifuta kesi moja inayowakabili viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), kutokana na kuchukua muda mrefu bila ushahidi wake kukamilika.
Hakimu Ame Msaraka Pinja alisema jana kuwa, anaifuta kesi hiyo kwa kutumia kifungu cha 209 cha makosa ya jinai.
Washtakiwa wa kesi hiyo ambayo ilikuwa ni moja kati ya tatu zinazowakabili ikiwa kwenye Mahakama hiyo na nyingine Mahakama Kuu, walikuwa wanakabiliwa na kesi ya kuhatarisha amani kwa kutoa lugha kali.
Ilipotajwa mara ya mwisho, Machi 19 mwaka huu upande wa mashtaka ulidai kuwa, upelelezi haujakamilika na mawakili wa utetezi walimwomba hakimu kuifuta kwa vile washtakiwa wako ndani muda mrefu.
Wakili wa washtakiwa hao, Salum Toufik na Abdallah Juma walimwomba hakimu kutokana na taratibu za Mahakama hususan makosa ya jinai, kesi inapofikia miezi mitatu na kuendelea bila upelelezi kukamilika inapaswa kufutwa.
Upande wa mashtaka, ukiongozwa na Khamis Jafar waliomba Mahakama kuwapa muda zaidi kutokana na kuchukua kipindi kirefu bila upelelezi kukamilika.
Washtakiwa hao ni Masheikh Farid Hadi, Mselem Ali, Mussa Juma, Azza Khalid Hamdan, Suleiman Juma, Khamis Ali na Hassan Bakari. Washtakiwa hao bado wanakabiliwa na kesi iliyopo chini ya Hakimu wa Wilaya, Khamis Rashid na washtakiwa wanne wapo nje kwa dhamana, huku watatu wakiwa rumande kutokana na kukabiliwa na kesi nyingine Mahakama Kuu. Washtakiwa watatu ambao walikwenda katika kesi hiyo wakitokea rumande ni Masheikh Farid, Juma Suleiman na Mussa Juma.
Mwananchi
3 comments:
dhulma ina mwisho wake haidumu na kesi hajafutwa ile ime trasfiwa kutoka mahakama mmoja kwenda inginewe sisi si watoto wadodo mungu atatulipia na narudia tena dhulma ina mwisho wake haidumu mwisho wa siku watatoke tu masheikh wetu bi izni lillahi amin
Kwa mujibu wa taarifa za kusoma ktk magazeti niliwah kusoma kua kesi ikifika miez 3 bila ushahidi inatakiwa ifutwe.
Sasa kama wameifuta ya mwanakwerekwe kwanini hawaifuti na ya vuga? Halafu na fidia kwa kesi ya mwanakwerekwe pia lazima itolewe.
kesi hajafutwa bwana eeeh wanataka kuwatupia watu mchanga wa macho wasione wanachotaka kufanya halafu wayafanye wanayo yataka huku wakizuga wananchi lakini mungu si athumani
kila lenye mwanzo halikosi mwisho na dhulma daima haidumu ina mwisho wake
Post a Comment