ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 12, 2013

Mahakamani akidaiwa kuiibia Serikali Sh153 mil

Aliyekuwa Mhasibu katika ofisi ya Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali, Godfrey Mbwilo (katikati) akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi akipelekwa kizimbani kwa tuhuma za wizi wa Sh150 milioni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana. Picha na Venance Nestory. 

Dar es Salaam. Aliyekuwa mfanyakazi wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Godfrey Mbwilo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  akikabiliwa na  tuhuma za wizi wa Sh153 milioni.
Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumain Kweka alidai kuwa mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka  jana mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando na Wakili wa  Serikali Tumaini Kweka alidai kuwa mshtakiwa alifanya makosa hayo kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu.
Kweka alidai kuwa  Agosti 2, 2011 katika ofisi za Mkemia Mkuu wa Serikali, akiwa mtumishi wa umma aliiba Sh40 milioni mali ya Serikali zilizofika kwake kulingana na nafasi yake ya ajira.
Katika shtaka la pili, Kweka alidai kuwa Septemba 5,mwaka huo katika ofisi hizo aliiba Sh45 milioni  mali ya Serikali zilizofika kwake kulingana na nafasi yake ya ajira.
Alidai katika shtaka la tatu kuwa anadaiwa kwamba Oktoba 5, mwaka huo katika ofisi hizo aliiba Sh40 milioni mali ya Serikali zilizofika kwake kulingana na nafasi yake ya ajira.
Katika shtaka la nne, mshtakiwa huyo anadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari 31 na Aprili 10,2012 ofisini hapo aliiba Dola za Marekani 18,000 mali ya Serikali. Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
Kweka alidai shtaka linalomkabili mshtakiwa linahusisha kiwango cha fedha Sh 153.8 milioni hivyo sheria iko wazi chini ya kifungu namba 148 (5) (e) cha Sheria ya Mwenendo wa mashauri ya jinai (CPA).
Wakili wa utetezi, Deiniol Msemwa alikubaliana na hoja za upande wa mashtaka na kudai kwamba wako tayari kutimiza masharti ya dhamana yatakayotolewa na mahakama. Kesi itatajwa Aprili 24, mwaka huu.
Mwanachi

1 comment:

Anonymous said...

Madhara ya matokeo ya kidato cha nne yameanza kuonekana kwa waandishi wa magazeti. Ukisoma aya ya kwanza yenye maandishi meusi zaidi, utaelewa kuwa mtuhumiwa aliiba pesa hizo katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.....