ANGALIA LIVE NEWS
Friday, April 12, 2013
POLISI KUJENGEWA NYUMBA
SERIKALI ya Zanzibar , imesema inajiandaa kujenga nyumba za makaazi kwa ajili ya askari wa Jeshi la Polisi, pamoja na vituo vya kufanyia kazi. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, aliyasema hayo jan wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni jaaku Hashim Ayoub, aliyetaka kujua kama serikali ina mpango wa kujenga nyumba hizo katika ukanda wa utalii.
Akijibu suala hilo Waziri huyo alisema ni kweli serikali inalazimika kuuona umuhimu huo baada ya kuona sekta ya utalii ni muhimu kwa pato la taifa na tayari imeanza kujenga nyumba hizo.
Alisema nyumba na vituo vya kazi kwa ajili ya askari Polisi tayari mradi huo upo ambao utekelezaji wake unafanywa kwa pamoja na wafadhili, mbali mbali kwa kushirikiana na wananchi.
Aidha, Waziri huyo alisema katika kuutekeleza mpango huo, hivi sasa wameweza kujenga kituo cha Polisi cha Nungwi, Kiwengwa na Paje ikiwa pamoja na kukamilisha ujenzi wa nyumba ya makaazi katika eneo hilo la Paje.
Alisema kazi hiyo inaendelea kufanyika katika kuyaangalia maeneo mengine ya ukanda wa utalii ili kuweza kujenga nyumba hizo mpango ambao unaenda sambamaba na kuimrisha ulinzi wa Polisi jamii.
Hata hivyo Waziri huyo, alisema katika kukabiliana ana hali hiyo, pia serikali katika ukanda huo, imeweza kuunda kikosi kazi cha ulinzi kwa ajili ya maeneo ya utalii kutokan ukanda wa pwani ya Mashariki biashara hiyo imeimarika.
Kuna mabadiliko yameanza kufanyika anakamilisha mfumo wa Baraza la Manispaa kwani likiyumba kidogo linaweza kusababisha kutokea kwa matatizo.
Serikali imeunda jopo la mawakili kupitia ripoti ya Kamati teule ya Baraza la Wawakilishi juu ya utendaji wa Baraza la manispaa ili kuona namna ya kulifanyia kazi ambapo hapo baadaea litafikishwa BLM Mawakili ambapo alisema imo katika hatua za mwisho kusajili wageni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment