BEKI wa Yanga, Mbogo Ladislaus, anatarajiwa kufanyiwa tena upasuaji katika eneo alilofanyiwa awali.
Awali beki huyo aliyekuwa na uvimbe katika shavu lake la kulia, alifanyiwa upasuaji wiki chache zilizopita, ambapo sasa zoezi hilo linaweza kufanyika tena.
Akizungumza na Championi Jumatano, Daktari Mkuu wa Yanga, Nassor Matuzya, alisema lengo la kurudia kumfanyia upasuaji huo ni kumrudishia muonekano mzuri kwa kupunguza ngozi iliyolegea.
“Unajua awali tulifanya zoezi la kuondoa ile nyama iliyokuwa imevimba, zoezi ambalo tulifanikiwa lakini sasa kidonda kinakaribia kuwa sawa, lakini tutalazimika kumfanyia upasuaji tena eneo lile ili kurudisha ngozi yake,” alisema
Matuzya na kuongeza:“Lile eneo tulilompasua bado halijarudi kama tunavyotaka na hii inatokana na ile ngozi ya eneo lile bado imetanuka.kama ilivyokuwa awali kabla ya kumpasua, sasa tutaikata ile ngozi iliyozidi ambayo ndiyo itaweza kumrudishia muonekano mzuri.
“Bado tunajipanga kuangalia muda sahihi wa kufanya zoezi hilo,”
alisema Matuzya ambaye alihusika katika oparesheni ya awali akiwa na madaktari wengine, iliyofanyika kwenye Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar.
Kwa upande wa Mbogo mwenyewe, anasema bado anaendelea kusikia maumivu kidogo na uvimbe wake bado upo ingawa umepungua kidogo.“Mpaka sasa bado sijaambiwa na daktari lini natakiwa kurejea uwanjani, lakini bado uvimbe haujapungua kutokana na sehemu yenyewe niliyopasuliwa kuwa na ngozi ngumu, hivyo maumivu yatachelewa kuisha lakini kama ngozi ingekuwa nyepesi, maumivu yangepungua haraka, hiyo ni kwa mujibu wa daktari aliyenifanyiwa upasuaji huu,” alisema Mbogo.
GPL
No comments:
Post a Comment