Dar es Salaam na Arusha. Mgogoro wa ardhi katika eneo la Loliondo umechafua hali ya hewa ndani Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki kumpinga waziwazi, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Mwigulu Nchemba na kusisitiza kuwa uamuzi wa Serikali kuhusu eneo hilo utabaki palepale.
Waziri huyo amesema kauli zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wakiwamo wabunge wa CCM, haziwezi kubadilisha msimamo wa Serikali.
Kauli hiyo inatofautiana na ile ya Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Mwigulu Nchemba aliyekwenda Loliondo mwishoni mwa wiki iliyopita na kuamua kuupeleka mgogoro huo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisema hatua hiyo inakiuka sheria na ina athari kwa wananchi wa huko.
Akizungumza kwa simu jana, Kagasheki ambaye pia ni Mbunge wa Bukoba Mjini (CCM), alisema Serikali imeamua kuchukua kilomita za mraba 1,500 kati ya kilomita za mraba 4,000 za eneo la Loliondo.
Alisema ilifikia uamuzi huo ili kulifanya eneo hilo kuwa pori tengefu kwa ajili ya kusaidia wanyama kuzaliana na kupata malisho, hatua ambayo inapingwa na wakazi wa eneo hilo.
Waziri huyo alisema kuwa Nchemba, ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi, anapaswa kuelewa kuwa Serikali haikukurupuka kuchukua uamuzi.
Alisema matamshi ya kiongozi huyo wa CCM hayawezi kuwa msimamo wa chama kwani viongozi hao walitumwa kwenda Loliondo kukusanya maoni na kisha kuyawasilisha kwenye vikao vyake halali na siyo kutumia mikutano ya hadhara kutoa uamuzi.
“Hayo maneno kama kweli yamesemwa na Nchemba, basi hayo ni mawazo yake na wala siyo msimamo wa chama. Mimi najua chama chetu kina taratibu za kujadili mambo na siyo kuanza kuzungumza nje ya vikao,” alisema na kuongeza:
Mwananchi
No comments:
Post a Comment