ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 3, 2013

MIMBA NI KIGEZO CHA KUOANA?-4

IMEKUWA vyema kwako kupata nafasi ya kuchota elimu hii hapa kwenye ukurasa wa marafiki wa All About Love. Wewe ni mwerevu kwa kuchagua gazeti hili ambalo limejaza vitu vingi vyenye kuelimisha na kuburudisha.

Nakwenda kumalizia mada yetu iliyodumu hapa kwa majuma manne mfululizo. Imekuwa mada ndefu lakini yenye mafunzo makubwa katika maisha yetu ya kila siku.

Tumejifunza mengi kuhusu mambo ya kuzingatia pindi marafiki wanapojikuta wameangukia katika mimba ambayo hawakuitarajia.Wiki iliyopita nilieleza japo kwa kifupi sana kuhusu uamuzi mwingine ambao hujitokeza kwa wasichana baada ya kupata mimba zisizotarajiwa. Wapo wanaowaza kutoa au kushawishiwa na wenzi wao kufanya hivyo.

Wiki iliyopita nilieleza japo kwa kifupi sana kuhusu uamuzi mwingine ambao hujitokeza kwa wasichana baada ya kupata mimba zisizotarajiwa. Wapo wanaowaza kutoa au kushawishiwa na wenzi wao kufanya hivyo.
Hapa ndipo nitakapoanza napo. Rafiki zangu, asikudanganye mtu kutoa mimba kuna athari nyingi - za moja kwa moja na za ndani kwa ndani zinazoweza kusababisha uchungu katika maisha yako. Twende tukaone...

ATHARI ZA KUTOA MIMBA
Kwanza ni kosa la jinai. Haikubakili kisheria isipokuwa kama daktari ameshauri kufanya hivyo kwa lengo la kuokoa maisha ya mama. Ukiachana na hilo zipo athari ambazo mwanamke anaweza kuzipata kwa kufanya kitendo hicho.
Wataalamu wamethibitisha kwamba, mimba inapoingia katika mji wa uzazi inapaswa kukaa hapo kwa kipindi cha wiki 36 – 37 ndipo kiumbe kitoke; kukitoa kabla ya muda huathiri mfumo wa uzazi kwa ujumla hasa kama daktari aliyefanya hatasafisha mji wa uzazi vizuri.

Kwa kawaida, kwa kuwa tendo lenyewe si halali, madaktari wengi wanaofanya vitendo hivyo, hufanya kwa harakaharaka kwa lengo la kujipatia fedha na si rahisi kufuatilia kwa undani na usahihi.
Kutokana na kosa hilo, mwanamke anaweza kupoteza damu nyingi na kupata maambukizi au kutoboka mfuko wa uzazi au maumivu makali ya tumbo. Uharibifu wa kizazi ukiwa mkubwa na tatizo likacheleweshwa kufikishwa hospitalini, kuna na hatari ya kuondolewa kabisa kizazi!

Mwanamke anayetoa mimba hupoteza mvuto (mwonekano) wake wa asili baada ya kutoa mimba – kwa sababu alikuwa na kiumbe kilichotakiwa kuzaliwa na yeye kukikatishia maisha, chakula cha mtoto (maziwa) kilikuwa tayari kuanza kuzalishwa, lakini kwa sababu kiumbe kitakuwa hakipo, mfumo mzima wa utengenezaji wa chakula hicho na mwili kwa ujumla wake huharibika.

Mwanamke ambaye ametoa mimba nyingi hasa zaidi ya tatu, anakuwa kwenye hatari ya kupata tatizo la mimba kutoka hapo baadaye. Pia kuna tatizo la kufedheheka kisaikolojia. Mwanamke aliyetoa mimba hujihisi mkosaji na mara nyingi hukumbuka kwamba, kama asingetoa mimba angekuwa na mtoto.
Hili hujitokeza zaidi ikiwa baadaye atapata tatizo la kutoshika mimba au kupata halafu zinatoka kabla ya kujifungua.

KWANINI YOTE HAYO?
Una sababu gani ya kujiingiza kwenye hatihati ya madhara makubwa kama hayo? Kwanini utoe kiumbe ambacho pengine umepangiwa hicho pekee katika maisha yako yote?
Kwanini ujiweke kwenye hatari ya kukosa mimba nyingine? Mimba kutoka hovyo na kutolewa kizazi? Kwanini yote hayo? Kipo kitu cha kufanya ili yote hayo yasikukute. Tuendelee kujifunza marafiki zangu.

USIDANGANYIKE
Kuna rafiki yetu mmoja alinipigia simu na kuniuliza: “Kaka Shaluwa nina mchumba wangu lakini amesema mpaka nishike mimba ndipo anioe. Unaonaje, nikubali?”

Unaonaje swali hilo? Inawezekana na wewe uko katika wakati mgumu kama huo na hujui cha kufanya, usijali upo mwongozo. Ndugu zangu, acha kudanganyika. Hakuna majaribio ya namna hiyo. Acha kucheza na maisha yako.

Kama anakupenda hawezi kuwa na haraka eti ya upate mimba kwanza ndipo akuoe! Unajuaje moyoni mwake kuna nini? Vipi akibadilisha mawazo? Kuna vipimo vya kuangalia uwezo wa mwanamke/mwanaume kushika au kusababisha mimba. Mnaweza kutumia kipimo hicho.

Asitokee mtu akakudanganya ukakubali kufanyiwa majaribio. Maisha yako yana thamani sana. Amka, zinduka usingizini, toa matongotongo na unawe uso wako!

FUATA USHAURI HUU
Ni vyema kujizuia kufanya ngono kabla ya ndoa. Kwa bahati mbaya vijana wengi wa siku hizi hawawezi. Sawa...kwa sababu tayari umeshaingia kwenye mapenzi ni lazima ucheze salama na uwe makini ili usije kuingia kwenye matatizo baada ya kupata mimba kwa ‘bahati’ mbaya

Njia bora na salama zaidi ya kuzuia kupata mimba ni matumizi ya kondom. Ikiwa mnaaminiana kiasi cha kutosha kwa maana ya kwamba tayari mmeshajuana afya zenu na pengine kwa matakwa yenu wenyewe hamtaki kutumia kinga hiyo, suala la kuangalia kalenda litamhusu sana mwanamke.

Upo utaratibu rahisi wa kujua siku zilizo salama na zile zenye hatari ya kupata mimba. Sasa hapo si lazima niandike kila kitu gazetini, uliza kwa wataalamu walio karibu nawe wakusaidie. Msichana usikubali maisha yako yaharibike kwa kupata mimba isiyotarajiwa.

Kumbuka kwamba, uamuzi wa kupata au kutopata mimba uko mikononi mwako mwenyewe. Kusoma maandishi haya ni kitu kimoja, kuyashika na kuyafuata ni jambo jingine lenye maana zaidi, AHSANTE SANA!!!

14 comments:

Anonymous said...

Hahahah Mada ya leo imwagusa wanawake wengi wa hapa DC, wanaojishikisha mimba ili waolewe.. Jibu ni acheni kujidanganya mwanaume wa siku hizi kama hataki kukuoa hata ukimzalia mia hakuoi..Na mifano mingi tu tunayo ya kina dada kubwagwa baada ya kujishikisha mimba na wanaume hutoka baruti hata sura ya mtoto hataki kuijua.. Jamani kina dada tusome na tujifunze kushika mimba sio sababu ya kuolewa ila tu kuzaa innocent children na kuwanyima haki ya familia.. tuacheni haka kamchezo kabaya , na kwavile no yenu inakuwa kila siku labda pafunguliwe darasa la kuelimishana. Mnataka mchezo tumieni kinga mtajikinga na maradhi vilevile..Kwanza kimaadili na kidini ni vibaya, aibu na dhambi kuzaa nje ya ndoa.. Kama unataka kuoelewa tumia njia ingine na sio kujishikisha mimba..That plan DONT WORK. Asante

Anonymous said...

Kitu kinacho nisumbua mimi sio mimba lakini hawa wanaume wanao tia wanawake mimba na kukimbia. Wewe mwanaume kama hukutaka mtoto kwa nini huja jikinga mweyewe. Yote haya yasinge kukuta kama na wewe ulitumia ur brain. Wewe mwanaume ulio acha mtoto hata haya huna?. Ndio mana maisha yako huta endelea. Utajikuta kila siku una matatizo.

Anonymous said...

The writer above why do you feel the need to always blame women? Where is your part in this it takes two. If you're not ready protect your self. When you get in bed with someone there's always a chance to create a baby. Everyone needs to grow up.

Anonymous said...

Ebu naomba niambie mwanaume gani alie muacha mwanamke na mbina jamaa akawa mwaname wa mana?jamani sema ukweli. mwanamme anae acha mtoto hana mana.

Anonymous said...

Wa mama na sisi tuacheni mambo ya kishamba. Sio lazima kama mwanaume hakutaki achana nae. Angalieni watoto wenu. Hawa wanaume wetu baadae watamtafuta mtoto. Hapo ndio wewe sasa mjibu. Wewe ulikiwa wapi Mimi nilivyo kua naangaika na mtoto?.

Anonymous said...

The topic ni kwamba usijishikishe mimba ili uolewe.. mwanaume anaweza kukutia mimba na akaoa kwngine na asikuoe.. acheni ujinga wanawake. Kama hataki kukuoa na wewe unajua ndio maana hujishikisha mimba..na kama unajua achana nae wanaume wa siku hizi kama hataki kukuoa hata ushike mimba mia hakuoiiii.. mnabaki kuwatumia watoto kumkomoa..Acheni upumbavu wanawake wa DC. Majira bure marekani.. Haujashika mimba mpaka unapokataliwa?

Anonymous said...

Hahahha weraweraaaa patamu hapa leo. hebu nikae mkao wa kula na bia baridi enheee

Anonymous said...

Wanaume wangapi hapa hapa DC wanadanganya wanawake. Ndio mana yanawakuta. na nyie wanaume pia acheni ujinga. Kama ulikua humtaki mwanamke kitu gani kime kupeleka pale?.

Anonymous said...

Mimi jamani nimetiwa mimba na jamaa alie nidanganya na sasa hivi nina mtoto baba yake hayupo. Nampenda mwanangu kupita yule mwanamme. Watoto wanakua. Mimi namshukuru mungu kila siku. Wanawake nawambia mwanamme akikukimbia sio lazima. Kama hakutaki muache. Hujui mungu anakutakia kitu gani. Sasa hivi mimi mimeolea na American man anampenda mwanangu kama wake. na huyu jamaa sina hata mtoto nae. Mwanangu sasa hivi anamiaka 5. sijamtafuta baba yake na sitamtafuta.

Anonymous said...

Mdau unaesema wanaume wa DC wanadanganya wanawake, wanake wengi wa DC hawajiheshimu, na wanaume hawaoi mwanamke asiejiheshimu. Sasa kama mnakutana kwenye starehe anakuona malaya tu wakupass time.. unapojishikisha mimba kwa kutaka kuoelewa ndipo unapochemsha. kulala na mwanamke sio kutaka kumuoa au kumzalisha ni moja katika starehe na huwa mnasemaga uongo munatumia majira.. Sasa Bottom line ni kuwa wacheni upumbavu huo mtaishia kulea peke yenu na kuolewa hamuolewi vilevile na jiji linakucheka kwa upumbavu wako. makurumbembe hayoo yanahangaika

Anonymous said...

kuchuna mabuzi, utapeli na kuishi town mnajua ila kinga za mimba hamujui? msidanganye watu munajishikishaga makusudi mscheew. halafu wademu deisgn hii wananiboaga kweli

Anonymous said...

Wanaume wote wanao jibu wanajulikana. Jamani wote hamna akili. Kama were. ulikuwa hutaki mtoto kwanini wewe mwenyewe huja tumia kinga.?.Kama umesha jua mwanamke mdanganyifu kitu gani kimekupeleka pale?. Elimu ni muhimu sana. Na nyinyi pia acheni ujinga. The writer above stated you just wanted a good time. Good time always gets you something you weren't ready for. Jamani naomba wote wanaume na wanaake tumieni akili. 5minutes of good time leads to slot of heartache. Just my opinion

Anonymous said...

Wanaume wa kibongo wanao ingia America enzi hizi wanajifanya wajuaji sana. Acheni ujuaji bongo marekani kuna kitu kinacho itwa sheria. Utajikuta unalipa child support mpaka ukome.mwanamke anakucheka all the way to the BANK.mwite malaya,mwite mjinga, mwiite kila jina. Lakini jiulize nani mjinga mimi au wewe?

Anonymous said...

Weweeee sawasawa!!!!!!!!.