“Ndugu wananchi wenzangu, ni lazima tusafishe mazingira yetu, asiyetimiza hilo atakuwa amekiuka sheria za afya. Hivyo akibainika atatozwa faini ya Sh 50,000 papo kwa papo au kifungo cha miezi sita jela ama vyote kwa pamoja, epukeni adhabu hizo kwa kutimiza wajibu huo wa kutunza mazingira,” alisema Rweyemamu.
Handeni. Serikali wilayani Handeni,Mkoa wa Tanga, imetangaza kwamba kaya itakayoshindwa kufanya usafi katika eneo lake, itatozwa faini ya Sh50,000 ama kutumikia kifungo cha miezi sita jela.
Sheria hiyo ilitangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu, wakati kielezea mikakati yake ya kufanya Miji ya Handeni kuongoza kwa usafi wa mazingira nchini.
“Ndugu wananchi wenzangu, ni lazima tusafishe mazingira yetu, asiyetimiza hilo atakuwa amekiuka sheria za afya. Hivyo akibainika atatozwa faini ya Sh 50,000 papo kwa papo au kifungo cha miezi sita jela ama vyote kwa pamoja, epukeni adhabu hizo kwa kutimiza wajibu huo wa kutunza mazingira,” alisema Rweyemamu.
Rweyemamu alisema kwamba kwa vile mji huo wa Handeni ndio unaopewa nafasi kubwa ya kuwa makao makuu ya mkoa mpya unaotarajiwa kuanzishwa, kwa kuugawa Mkoa wa Tanga, ni bora wakauweka katika mazingira ya usafi.“Mji wa Handeni unapewa nafasi kubwa ya kuwa makao makuu ya Mkoa mpya unaotarajiwa kuanzishwa. Kutoka Kilindi, Pangani ama Korogwe, katikati yake ni Handeni na pia hata sifa unazo kwa kuwa na ardhi ya kutosha, sasa tuimarishe usafi katika maandalizi haya,” alisema Rweyemamu na kuongeza kuwa.
Mkuu huyo wa wilaya alimuagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, Thomas Mzinga, kuhakikisha anafanya mabadiliko kwa kusimamia usafi katika kila kaya, kwa kuwachukulia hatua wakaidi.
No comments:
Post a Comment