ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 10, 2013

Mtaala wa somo la historia haujafutwa Zbar

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali juma Shamuhuna.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema haiwezi kumfukuza Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Msingi kutokana na wanafunzi kutosomeshwa somo la historia kinyume na maelekezo ya mitaala ya elimu Zanzibar.

Msimamo huo umetolewa leo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali juma Shamuhuna wakati akijibu swali lililoulizwa na Mwakilishi Jaku Hashim Ayoub wa Jimbo la Muyuni aliyetaka kujua ni kwanini somo la historia halifundishwi katika shule za msingi Zanzibar .
Waziri Shamhuna alisema walimu wasiofundisha masomo hayo ndiyo wanaostahili kufukuzwa kazi kwa vile wanakwenda kinyume na mitaala ya elimu Zanzibar kwa vile Serilali haijafuta somo la histria kutofundishwa kwenye shule za msingi visiwani humo.

“Mkurugenzi hastahili kufukuzwa kazi,bali wanaopaswa kufukuzwa ni walimu ambao inawezekana hawafundishi kwa kutolipenda somo hilo,.uvivu au uzembe lakini Seriklali kamwe haijafuta mtaala wa somo la historia”Alisema Shamhuna.

Alisema somo hilo lina umuhimu mkubwa katika kuwaeleimisha vijana kuhusu historia ya nchi yao na maendeleo ya dunia kwa ujumla wake ili kuwasaidia wao wenyewe kujitambua wanakotoka ,walipo na wanakoelekea.

Alieleza kuwa lengo la serikali kuwa na vituo vya utamaduni yakiwemo makumbusho ya asili ya Forodhani,Beitil el ajib na kituo cha uhifadhi wa nyaraka ni kulinda historia ya kweli pamoja na kusaidia kazi za utafiti kwa maendeleo ya wanafunzi viziwani Zanzibar.

Awali Mwakilishi Jaku alitaka kujua somo la historia limelkuwa halifundishwi katika shule mbalimbali za Unguja na Pemba na kuungwa mkono kauli hiuyo na Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani Hija Hassan Hija ambaye aliasema watembeza watalii wengi Zanzibar hawajui historia ya Zanzibar.

Alisema kwa kuwa somo la historia haliajaondolewa katika mitaala,Mkurugenzi alipaswa kuondolewa kwa kushindwa kusimamia majukumu yake ya kiajira na kusibabisha vijana wengi kushindwa kujua historia ya nchi yao.

CHANZO: NIPASHE

No comments: