Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchikavu na Majini (Sumatra), Ahmad Kilima (kulia), akimkabidhi vifaa vya vipima ulevi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, jijini Dar es Salaam jana.
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchikavu (Sumatra) imekabidhi kwa Jeshi la Polisi vifaa 2,000 vya kupima ulevi kwa madereva ili kupunguza ajali za barabarani nchini.
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa Sumatra, Ahmed Kilima, alisema usafiri wa barabarani ni muhimu kwa jamii lakini ni ukweli usiopingika kuwa ajali za barabarani zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku na kwamba ajali hizo mara nyingi zimekuwa zikisababishwa na makosa ya kibinadamu.
Alisema miongoni mwa makosa hayo ni ubovu wa vyombo vya usafiri na hali ya miundombinu kuwa mbaya, jambo ambalo limekuwa kikwazo kikubwa katika juhudi za serikali na wananchi kuleta maendeleo.
Alisema pamoja na juhudi kadhaa zilizokwisha chukuliwa katika kukabiliana na janga la ajali nchini lakini bado hali si nzuri.
Kilima alisema bado kuna umuhimu wa kuendelea na juhudi za kupunguza ajali na ndiyo maana Sumatra kwa kushirikiana na Taasisi ya Bico ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, iliamua kufanya utafiti wa kina wa tatizo la ajali za barabarani kwa upande wa Tanzania Bara.
Alisema matokeo ya utafiti huo yalionyesha kwamba ajali nyingi zinasababishwa na makosa ya kibinadanu ambayo ni uzembe wa madereva wa mwendo kasi, kuzidisha uzito, uchovu wa madereva, kutozingatia sheria, kanuni za usalama barabarani na ulevi.
"Kwa kuangalia uwiano wa mchango wa kila sababu katika kusababisha ajali, imebainika kuwa makosa ya kibinadamu yanachangia kwa asilimia 76, wakati hali ya gari inachangia kwa asilimia 16, na asilimia 8 inachangiwa na hali ya miundombinu barabarani," alisema Kilima.
Akipokea vifaa hivyo, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema, aliwataka wananchi kushirikiana na Sumatra pamoja na jeshi hilo katika kupambana na madereva walevi ili kupunguza ajali nchini.
Alisema wananchi wana nafasi kubwa katika vita hivyo kwa kutoa taarifa za kitendo cha uhalifu katika sehemu husika.
Katika hatua nyingine IGP alisema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Sumatra, makamanda wa polisi wa wilaya na mikoa, kamati za ulinzi na usalama, limeandaa mpango maalum wa kuzisajili pikipiki zote zinazotumika kwenye biashara ya Bodaboda kwa kuzipa vibao maalumu vya namba ili ziweze kutambulika kirahisi.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment