Askari anayedaiwa ni wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) anadaiwa kuua dereva wa bajaj kwa kutumia bunduki katika maeneo ya Kawe Shoko, jijini Dar es Salaam.
Tukio la kuuawa kwa kijana huyo jana jioni inadaiwa lilitokana na kutokea mabishano kati yake na mwanajeshi huyo wakati ikipita eneo ambalo raia hawaruhusiwi kupita.
Vurugu kubwa zilitokea katika eneo hilo baada ya kutio hilo huku vijana wenzake marehemu kukusanyika kuhoji sababu za kuawa kwa mwenzao.
Mashuhuda walisema kuwa baada ya askari kuho kumpiga risasi kijana huyo na kumuua, mwili wake ulichukuliwa na gari la kubebea wagonjwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo.
Mwandishi wa NIPASHE alipofika eneo hilo majira ya saa 2:15 usiku, alikuta wananchi wakikimbia hovyo na huku milio ya risasi ikisikika.
Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, aluthibitisha alikiri kutokea kwa tukio na kuongeza kuwa bado Jeshi la Polisi linafuatilia ili kupata taarifa zaidi.
Jaji mstaafu, Ernest Mwipopo, amefariki dunia na watu wengine wanne kujeruhiwa baada ya gari dogo alilokuwa akisafiria kutoka Iringa kwenda Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka katika eneo la Mkata, Barabara ya Morogoro-Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Alisema ajali hiyo ilitokea jana majira mchana na kwamba marehemu na watu wengine watano, akiwamo dereva walikuwa katika gari lenye namba za usajili T 691 AYL wakitokea Iringa kwenda Dar es Salaam.
Shilogile alisema walipofika eneo la Mkata, gari hilo lililoonekana kuwa katika mwendo mkali, lilipasuka tairi ya nyuma kulia na kuanza kuyumba barabarani na baadaye kidogo ilipasuka tairi ya mbele kushoto na kupinduka mara mbili kabla ya kuwaangukia wauza mkaa wanaofanya biashara zao pembezoni mwa barabara hiyo kuu eneo la Mkata.

Jaji Mwaipopo afariki ajalini

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment