Super Nyamwela
“Nimeanza kuimba hivi sasa, lakini sifikirii kama siku moja nitaacha kucheza muziki, hiyo ni fani yangu. Nina umri wa miaka 32 na watoto wakubwa tu, lakini bado sijafikiria kuachana na fani yangu,” alisema Nyamwela
Mcheza shoo wa bendi ya Extra Bongo nchini Hassan Musa Mohamed maarufu kama Super Nyamwela (pichani kushoto) mwenye umri wa miaka 32 amesema ingawaje hivi sasa umri wake umeenda hawezi kuacha kusakata rhumba.
Nyamwela mwenye maelfu ya mashabiki katika muziki wa dansi, alisema kwa sasa ameanza kuimba lakini hawezi kuacha asili yake.“Nimeanza kuimba hivi sasa, lakini sifikirii kama siku moja nitaacha kucheza muziki, hiyo ni fani yangu. Nina umri wa miaka 32 na watoto wakubwa tu, lakini bado sijafikiria kuachana na fani yangu,” alisema Nyamwela mwenye mtoto anayesoma kidato cha pili na wengine watatu ambao ni wadogo.
Nyamwela aliyekua katika fani hiyo kwa miaka 20 sasa, alisema kinachomuuma sana ni kitendo cha yeye kufundisha vijana wadogo ambao huwa wanakuwa wazuri zaidi yake katika kusakata dansi lakini huwa wanaachana na fani hiyo baada ya muda.
“Mimi ni mwalimu ninayewafunda vijana na madansa wa kike wengi tu, lakini kinachoniuma ni vijana wengi kutokukua katika fani hii, wengi wao huachana nayo na kuamua kufanya mambo mengine licha ya kuwa na uwezo,” alisema Nyamwela anayetarajia kufungua chuo maalumu kitakachofundisha fani hiyo.
Mnenguaji huyo aliye katika bendi ya Extra Bongo, hivi sasa ameimba nyimbo kama Bakutuka na Ufisadi wa Mapenzi ambazo zimepokelewa vizuri na mashabiki
No comments:
Post a Comment