ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 19, 2013

‘Pamoja na kuua wengi hatuwezi kuzuia bodaboda’

Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Ni kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyoitoa bungeni alipojibu maswali ya wabungeUsafiri wa bodaboda umeshamiri maeneo mengi ya mijini na vijijini ambapo pamoja na kuwapo kwa matukio mengi ya ajali, lakini unasaidia kupunguza kero ya usafiri nchini.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema si rahisi Serikali kupiga marufuku usafiri wa pikipiki kubeba abiria maarufu kama bodaboda licha ya kutambua kuwa ni sababu kubwa ya ajali na vifo vya watu wengi.Badala yake, Pinda alisema kinachofanyika ni kutoa elimu kwa kutumia vyombo mbalimbali hadi vijijini walikosambaa, kwa kuwatumia polisi, vyuo vya Veta na asasi za kiraia ili kupunguza ajali hizo.Kipindi cha mwaka jana pikipiki ziliua watu 771 kwa ajali 4,637 ambapo watu wengine 4,562 walijeruhiwa.
Mwaka 2011 ajali za pikipiki zilikuwa 3,326 na kusababisha vifuo vya watu 594 na kujeruhi wengine 3,034.Pamoja na ajali hizo, Pinda alisema Serikali inashindwa kuzisimamisha pikipiki kwa sababu kwa upande mwingine zinasaidia.Pinda alitoa majibu hayo wakati anajibu swali la Magdalena Sakaya (Viti maalumu-CUF) aliyetaka kujua tamko la Serikali kuhusu usafiri huo ulioruhusiwa nchini kwa sheria ya Bunge lakini matokeo yakawa kinyume na matarajio.

Kwa mujibu wa Sakaya, badala ya kuleta neema iliyotarajiwa usafiri huo umegeuka balaa kwa kusababisha vifo na ulemavu wa vijana wengi nchi nzima.Alisema waendeshaji wa pikipiki wengi hawafuati sheria, ni wajeuri hivyo akapendekeza wapewe kozi ya miezi mitatu ili kuwaweka sawa.
Mwananchi

No comments: