Bilal ni Mtanzania mzanzibari licha ya kuwa engineer wa umeme na Dj pia ni mpishi mzuri sana wa Biryani, Biriani ni wali unaopikwa kwa ustadi sana siyo kila mtu anaweza kupika chakula hicho kutokana na vikorombwezo vingi vinavyo tumika kukamilisha mpango mzima wa chakula cha biriani. ndio maana Bilal ni bingwa kama unavyomwona kwenye picha akitoa maelezo juu ya upikaji wa biryani mbele ya ukodak wa vijimambo ulivyo piga hodi nyumbani kwa Bilal Brooklyn. NY.
Sifa na kazi ya biriani unatakiwa kukoroga mwanzo mwisho vikorombwezo vyake hili kukamilisha radha ya biryani.
Bilal akikoroga mchanyato unaokamilisha mapichi ya biryani
Yuko makini sana hapa kuakukisha kitu kitakacho tokea hapa kiwe chenye ubora wa TBS
Vikorombwezo vimetimia kilicho kuwa kimebakia hapo ni kuwekwa nyama na mchele tu hili biriani liwe tayari lakini sifa yake ukilipika leo liliwe next day hili kupata radha yake
1 comment:
Vijimambo NY Ebra sasa tujue vipi? linatwa birian au biryani? pia kuna sehemu umeandika hili au ili unatuchanganya na unatoa uhalisi wa habari kwa kukoseakosea kuandika kiswahili fasaha.
Mdau
Post a Comment