Hatuahiyo pia imekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya wananchi wa mkoa huu.
Profesa Lipumba aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa siku moja uliolenga kuzungumzia ajenda ya maendeleo kwa wote katika mkoa wa Tanga.
Mada kuu katika mkutano huo ililenga kuzungumzia hali ya uchumi mkoani humu.
Profesa Lipumba alisema inashangaza kuona mkoa huo ambao ulitambulika duniani kwa kuzalisha zao la mkonge kwa wingi, bado upo nyuma kiuchumi. Alisema takwimu za mwaka 2009 zinaonyesha kuwa bei ya mkonge katika soko la dunia imefikia dola za 2,632 za Marekani kwa tani. Alisema katika mwaka 1964, tani zipatazo 234,000 za mkonge zilizalishwa nchini ambapo asilimia 60 zilitoka mkoani Tanga.Profesa Lipumba alisema zao hilo kwa sasa limeanza kufufuka na kuimarika katika soko la dunia.
“Pamoja na kuporomoka kwa bei ya mkonge katika soko la dunia kwenye miaka ya hivi karibuni, zao hili la biashara limeimarika hivyo ni wakati mwafaka kwa serikali na wadau kuhamasisha wakulima wadogo na wakubwa kuzalisha kwa wingi hasa kwa kuzingatia uhakika wa soko upo,”,alisisitiza.
Hata hivyo, Profesa Lipumba alisema anashangazwa na namna ambavyo uchumi wa mkoa wa Tanga umekuwa ukidorora siku hadi siku licha ya kuwa na rasilimali nyingi ikiwamo ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo, madini, viwanda, bahari na bandari.
Alisema kimsingi maendeleo ni pamoja na wananchi kuwa na uhakika wa kupata huduma bora za afya elimu, ajira, uwezo wa kumudu maisha kila siku sambamba na uzalishaji wa chakula kwa wingi kwenye sekta ya kilimo.
Profesa Lipumba alisema uzalishaji wa chakula kwa wingi, kutasaidia kupunguza mfumuko wa bei na kushusha gharama za maisha.
Kuhusu sekta ya elimu alisema bado hajilenga kumwezesha kijana kukabiliana na changamoto za maisha ili hatimaye ashiriki shughuli za kisiasa na kijamii.
Nao baadhi ya wadau walioshiriki mkutano huo, walisema ni wakati mwafaka kwa wakazi wa mkoa wa Tanga kuhoji sababu za kuendelea kudorora kwa uchumi wa mkoa huo.
No comments:
Post a Comment