WanaJumuia,
Kwa niaba ya familia ya Marehemu Bibi Loveness Kisaka, napenda kutoa shukurani za dhati kwa wale walioshiriki katika kufariji familia kwa njia moja au nyingine katika kipindi cha msiba.
Kwa kweli familia ya Marehemu ilifarijika sana na inatumaini kwamba jumuia yetu itaendelea kuwa na upendo na mshikamano tuliouonyesha kwao kwa siku zote. Familia inashukuru kwa yote ikiwa ni pamoja na dua, kupiga simu, kwenda kuwatembelea, na kuchangia gharama za kumsafirisha marehemu kwenda Tanzania kwa maziko.
Katika shukran hii, familia ya Marehemu inapenda kuwaalika Wanajumuia katika misa fupi ya kutoa shukran Jumamosi hii Tarehe 20-April-2013 nyumbani kwa Mzee na Mama Bundu (Mama Bundu ni binti ya Marehemu) kuanzia saa nane mchana (2 pm). Anuani yao ni kama ifuatayo:
232 Manzanila Way
Oceanside, CA 92057
Kwa taarifa zaidi tafadhali jisikie huru kumpigia Mama Bundu (760) 687-3546.
Na kwa wale watakaoshindwa kuhudhuria Jumamosi hii, tafadhali fungua na kusoma ujumbe wa shukran uliambatanishwa kwenye email hii ambao unatoka kwa familia ya Marehemu.
Mtumishi Wenu,
Rabia Dahal
No comments:
Post a Comment