Advertisements

Thursday, April 18, 2013

SI HAKI KUANZA KUIHUKUMU BRIGEDI MAALUM-BAN KI MOON

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akiwa katika mkutano na Waandishi wa Habari wa Chama cha Waandishi wa Umoja wa Mataifa siku ya jumatano, katika mkutano huo, pamoja na mambo mengine, Katibu Mkuu alieleza imani yake kubwa kwa Brigedi Maalum itakayopelekwa Mashariki mwa DRC kwamba itatoa mchango mkubwa sana katika uimarishaji wa amani na usalama na hivyo haikua haki kuanza kuihukumu kabla hata haijafika eneo la jukumu. Mwezi uliopita Baraza Kuu la Usalama lilipitisha Azimio ambalo pamoja na mambo mengine liliridhia kupelekwa kwa Brigedi hiyo maalum na imeipa Brigedi dhamana na uwezo pale itakapolazimika kutumia nguvu kuyadhibiti makundi ya wanamgambo wenye silaha ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiendelea kulifanya eneo hilo kutokuwa na amani na usalama wa kudumu.

Na Mwandishi Maalum
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon,  amesema si haki kuanza kuihukumu na  kutupia lawama Brigedi  Maalum  (Intervention Brigade )inayotarajiwa kupelekwa   Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( DRC) hata kabla Brigedi hiyo    haijafika eneo lake la jukumu. 
Kauli hiyo ya Katibu Mkuu, imefuatia swali aliloulizwa na mmoja wa waandishi  kutoka  Chama cha Waandishi wa Umoja wa Mataifa alipokutana nao siku ya  jumatano, ambapo alizungumzi masuala  mbalimbali muhimu yanayoendelea hivi sasa duniani katika nyanja za   usalama, uchumi na maendeleo.
Katika swali lake, mwadishi huyo aliuliza kuwa,  baada ya Baraza Kuu la Usalama, kupitisha Azimio ambalo limeridhia kupelekwa kwa Brigedi  maalum kumejitokeza   maoni tofauti kutoka kwa  makundi mbalimbali ya jamii, yakiwamo ya wanawake.
Maoni   hayo ni pamoja na kuwa  ,   upelekaji wa  brigedi hiyo  maalum kunaweza kuchangia  uzotoraji zaidi wa  amani na usalama na hivyo  kuhatarisha zaidi   haki za binadamu zikiwamo za wanawake. Na  nini  yalikuwa  maoni yake    (Katibu Mkuu )  kuhusu  brigedi hiyo  na mstakabali wa haki za wanawake.
Akijibu swali hilo,   Ban Ki Moon, alisema.  “ Azimio  lililopitishwa na  Baraza Kuu la Usalama mwezi uliopita kuhusu upelekeaji wa brigedi mpya  kwanza ,ni   Dhana mpya   lakini pili huu  ulikuwa uamuzi muhimu sana. Si haki kwa kweli,   kuanza  kuihukumu na kuitupia lawama    brigedi hiyo  hataka  kabla haijafika DRC”.

Na kuongeza. “Tuko katika maandalizi makubwa ya kufanikisha upelekaji wa brigedi hii maalum . Ni matumaini yangu kwamba  brigedi  itatoa mchango mkubwa sana katika  uimarishaji wa amani na usalama katika DRC”.
Akaongeza kwa kusema   upelekaji wa    brigedi  hiyo  unaimarisha uhakika wa hatimaye kupatikana  amani, usalama na  ulinzi wa raia,  pamoja na kulinda haki za binadamu zikiwamo za wanawake.
Akafafanua zaidi kwamba, mwishoni mwa Mwezi ujao ( Mei)anatarajia kwenda kuhudhuria mkutano wa Kilele wa wakuu wa nchi na  serikali wa Umoja wa Afrika ( AU).
 Na kwamba wakati wa mkutano huo atakutana na    kufanya mazungumzo na viongozi  11  na wadhamini wanne ambao mwezi  February 2013 huko Addis Ababa, Ethiopia, walitia saini  Mpango mpana wa  kisiasa wa  Umoja wa Mataifa wa amani, usalama na   ushirikiwano wa maendeleo katika DRC na eneo la Maziwa Maku
Itakumbukwa kwamba mwezi Marchi mwaka huu,   Baraza Kuu la Usalama katika tukio la kihistoria lililoambatana na maamuzi magumu lilipitisha kwa kauli moja azimio namba 2098 ( 2013) ambalo pamoja mambo mengine, liliidhinisha upelekaji wa Brigedi Mpya katika DRC.
 Brigedi maalum itaundwa na wanajeshi  3,069 kutoka Tanzania, Afrika ya  Kusini, na Malawi  itakakuwa na uwezo,  pale itakapolazimika, wa kuyakabili, kuyadhibiti na kupokonya silaha makundi ya wana mgambo yenye silaha katika  nchi  hiyo hususani katika eneo la Mashariki. 

No comments: