Shule ya Msingi mvumi
Wanafunzi wa shule mbali mbali wakiwa wamekaa chini huku wakisoma,kwakweli inasikitisha sana naamini mimi na wewe tunauwezo wa kusaidia hili kulingana na nafasi, zetu,hizi shule zipo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma. kama unafikiri unaweza kusaidia japo kidogo hasa sisi Watanzania tuishio ughaibuni na nyumbani tafadhali wasiliana kwa barua pepe na
Marafiki wa Elimu Dodoma, Ibrahim Cahogo
Shule ya Msingi Chamwino.
Shule ya Msingi Chalula.
Shule ya msingi Mvumi
Kwa kitabu hiki hawa watoto wanasoma nini na wataelewaje? Tutafute kwanza kipande kilicholiwa na mchwa ndipo tupe kazi ya kujibu maswali! Ama kweli tuzisubiri fedha za rada zinaweza kupunguza tatizo hili. Shule ya Pahi iko Mkoani Dodoma katika Wilaya ya Kondoa
Kibao kinachokataza kutumia lugha ya kirangi na kusisitiza kutumia kiswahili katika shule ya sekondari Chagaa iliyoko Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma. Wanafunzi wa shule hiyo hutumia zaidi lugha ya Kirangi kuliko Kiswahili na Kiingereza kwao ni majaaliwa ya Muumba.
Humu ni ndani ya Bweni la wavulana katika shule ya Mbabala Sekondari iliyopo katika Manispaa ya Dodoma.
Picha na Marafiki wa Elimu Dodoma(MED)

7 comments:
duu na ndio kwa wabunge na mawaziri tuseme ndipo serekali ilipo.
Ndugu Ibrahim Cahogo, pamoja na wazo lako zuri, halitafua damu hadi tutakapo wawajibisha wabunge watunge sheria kubadilisha mfumo mzima wa elimu. Wao wanapoendelea "kutesa" huko Dodoma, hutumia jengo lenye air condition na huku shuleni jirani kuna watoto wanalazimika kuwa ktk mazingira yasiyokidhi hali ya kujifunza. Hii ni dhambi ya mauti.
Nimelia sana nilipoona watoto wamekaa chini hawana madawati!!! Jamani, wakwaapi mawaziri, wabunge wanalilia marupurupu wakati kuna watoto wanakaa chini darasani? Rais Kikwete unalionaje swala hili mkuu? duu!
Inatisha Ila badala ya kulia ungesaidia hata kuchangia madawati
Mbona unalenga sehemu moja tu,?lete breakdown za mahitaji na gharama. Halafu pia hali ikoje mikoa mingine? Wapi wana hali mbaya zaidi? Fanya comparison hizo na rate za kufaulu wanafunzi,kiwilaya au mkoa. Hapa more research inatakiwa. Halafu sisi wa ughaibuni,tukitaka kusaidia,tunaomba contacts za sehemu yanakouzwa madawati.
Ni kweli kama wadau walvyosema, kama picha hizi hazikutoi machozi basi wewe una moyo wa jiwe kama watawala wetu. Mimi sichangii cho chote hadi wananchi wa Dodoma watakapoonesha angaa nia kidogo kuwa wanakataa watawala waliowafikisha hapa!!!
huyu Rais kikwete namawazili wote ni walewale,wazazi ndiowaliochangua kiogozi huyu haaaaaaa.
Post a Comment