Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta, anaapishwa rasmi leo huku marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakitazamia kuwa miongoni mwa wageni mashuhuri kwenye sherehe hizo.
Uhuru na mgombea mwenza wake, William Ruto, walichaguliwa katika uchaguzi wa Machi 4 mwaka jana kwa zaidi ya kura milioni 6.13 na hivyo kumshinda mpinzani wake Rail Odinga, aliyepata kura milioni 5.3.
Uchaguzi huo ulifuatiwa ule wa Desemba mwaka wa 2007 uliomalizika kwa ghasia za kikabila na kusababisha zaidi ya watu 1,000 kupoteza maisha na wengine kupoteza makazi.
Kuhusu sherehe, maofisa wa Serikali ya Kenya, walisema zinatazamiwa kuhudhuriwa na viongozi kadhaa barani Afrika na kwamba baadhi yao walianza kuwasili nchini humo tangu jana.
Viongozi hao ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete ambaye ameambatana na maofisa kadhaa wa Serikali yake.Wengine ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Rais Omar al-Bashir wa Sudan.
Hata hivyo, kumekuwa na sintofahamu kuhusu kuhudhuria kwa kiongozi huyo wa Sudan anayetakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inayomtuhumu kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu katika Jimbo la Darfur.
Maofisa wa Serikali ya Kenya wamesema kiongozi hayumo katika orodha ya waalikwa katika sherehe za kumuapisha Rais Kenyatta.Lakini gazeti Akbar al-Youm,lilisema kuwa rais Bashir alitazamiwa kuwasili nchini Kenya kuhudhuria sherehe hizo na baadaye kwenda Chad kuhudhuria mkutano wa Ukanda wa Kijani.
Hii si mara ya kwanza kwa rais wa Sudan kuzuru nchini Kenya mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2010 wakati rais anayemaliza muda wake Mwai Kibaki, alipomwalika kwenye sherehe za kupitishwa katiba mpya.
Kitendo hicho kilishutumiwa vikali ikiwemo Jumuiya ya Kimataifa iliyookosoa Kenya kuwa inakiuka makubaliano ya kimataifa inayotaka nchi wanachama kutoa ushirikiano kwa mtuhumiwa yoyote anayewasili nchi husika.
Changamoto kwa Uhuru Kenyatta
Uhuru Kinyatta ambaye ni miongoni mwa viongozi wenye umri mdogo katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mtihani wake wa kwanza ni kurejesha umoja wa kitaifa miongoni mwa raia wa Kenya ambao wamegawanyika kwa misingi ya kikabili.
Atakabiliwa na wakati mgumu wa kukubalika katika baadhi ya majimbo hasa katika maeneo ambayo yanatajwa kuwa ngome muhimu ya mpinzani wake Raila Odinga.
Mwananchi
1 comment:
mafisadi siku zote wanakwenda mbele pamoja na watoto wao na vizazi vyao ukijua historia ya chalii yani watanzania mngeshangaa
Post a Comment