Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Marceline Magesa (kulia) akizungumza katika hafla ya uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaam- Bagamoyo leo jijini . Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba watu 300 , kitagharimu shilingi7.91 bilioni.(bilioni7.91 za tz).Pichani kutoka kulia ni Waziri wa Uchukuzi Dkt,John Magufuli,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadick, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi , Balozi Herbert Mrango.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Marceline Magesa (mwanamke) , na mwakilishi wa kampuni ya JOHS GRAM HANSSEN A/S ya Denmark Andreas Gottrup wakiweka saini mkataba wa ujenzi wa Kivuko cha Dar es Salaam- Bagamoyo leo jijini Dar es Salaam, katika hafla iliyoshuhudiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (aliesimama katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadick(alie vaa shati la kitenge) Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mh, Johnny Flinto (mzungu aliesimama mstari wa nyuma). Pamoja na watendaji wakuu wa Wizara ya Ujenzi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sadick Mecky (kulia) akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa Kivuko cha Dar es salaam – Bagamoyo. Kivuko hicho kitagharimu shilingi 7.91 bilioni za kitanzania. Mwengine ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kulia) akiongea na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mh. Johnny Flinto,katika sherehe ya uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaa- Bagamoyo (April 25, 2013).
Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya TEMESA, Prof. Idrisa Mshoro (kulia) akimueleza jambo Mwakilishi wa kampuni ya JOHS GRAM HANSSEN A/S ya Danmark , Andreas Gottrup wakati wa sherehe za uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaam- Bagamoyo jijini Dar es Salaam(April,25,2013).
waziri wa ujenzi Dr. John magufuli akiongea ktk hafla
1 comment:
Huu uwekaji wa mikataba hadharani maana yake nini wakati hatujui yaliyo ndani ya hiyo mikataba? Kama bado wanafanya ujinga ule ule wa mikataba ya ulaghai tutajuaje?
Post a Comment