Maghorofa matatu watu wahamishwa
Mkandarasi diwani wa CCM mbaroni
Wakati miili ya watu waliokufa katika jengo la ghorofa 16 lililoporomoka Ijumaa ya wiki iliyopita jijini Dar es Salaam iliyopatikana ikiwa imefikia 29, serikali imeamuru watu waliopo katika maghorofa mengine matatu yaliyopo jirani na ghorofa hilo kuhama mara moja kwa sababu hayapo katika hali ya usalama.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema majengo hayo yanayomikiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), wapangaji wake wanatakiwa kuondoka ili uchunguzi ufanyike kubaini kama yana uimara unaotakiwa.
Sadiki alisema majengo hayo yanaweza yakawa yamepata mtikisiko mkubwa kutokana na kuwa karibu na ghorofa lililoanguka na ghorofa moja kati ya hayo matatu tayari limeonyesha dalili za kuwa na nyufa.
“Nimewaagiza Shirika la Nyumba la Taifa kuwaondoa wapangaji wake wote waliopo karibu na ghorofa lililoporomoka ili uchunguzi wa majengo hayo ufanyike,” alisema Sadiki.
Alisema NHC watagharamia gharama zote za mazishi kwa maana ya jeneza, sanda na kusafirisha miili ya waliokufa kupelekwa katika maeneo mbalimbali ya nchi.
WALIOKUFA WAFIKIA 29
Awali akizungumza na NIPASHE jana mchana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema kuwa idadi ya watu waliokufa imefikia 28.
Hata hivyo, baadaye jioni Sadiki aliiambia gazeti hili kuwa idadi hiyo imeongezeka na kufikia watu 29 na kwamba hadi saa 1:10 usiku zoezi la kutafuta miili zaidi lilikuwa linaendelea.
Sadiki alisema zoezi hilo litaendelea ili kuhakikisha kwamba linakamilika kwa siku ya jana.
WALIOKAMATWA WAONGEZEKA
Katika tukio lingine; Kamanda Kova alisema kuwa idadi ya watu wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo imeongezeka na kufikia wanane.
Aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni mmiliki wa ghorofa hilo, Raza Husein Damji (69) na mtoto wake, Ally Raza Damji (31) ambaye alikuwa akishirikiana naye.
Wengine ni wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Mhandisi Ogare Salu, Mhandisi wa Majengo , Goodluck Mbagaga, na Mkaguzi wa Majengo, Wilbroad Mugyabusu.
Mkandarasi wa Kampuni ya Lucky Construction iliyokuwa ikijenga jengo hilo na ni Diwani wa Goba (CCM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Ibrahim Mohamed Kisoki.
Pia wamo Zonazea Anage Oushadada (53), ambaye ni Mhandisi Mshauri na Mohamed Abdulkarim (61), mshauri wa kujitegemea aliyekuwa akitumiwa na mmiliki wa jengo.
Alisema watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo kama wangekuwa makini, janga hilo lisingetokea na kwamba wakati wakiendelea kuhojiwa, Jeshi la Polisi nalo litaendelea kuchunguza.
Kova alisema wakati wa zoezi la kuokoa watu waliofukiwa na kifusi cha jengo hilo likiendelea, walikuta nondo na mifuko kadhaa ya saruji ambayo ilikuwa imefukiwa kabla ya kutumika.
Alisema kutokana na tukio hilo, serikali imemua kuchukua majina ya watu ambao ni wataalam wa masuala ya majanga ili kunapotokea janga wanaitwa haraka kusaidia.
Kamanda huyo alitoa onyo kwa watu wanaochukua nondo zinazotupwa pamoja na kifusi kutoka katika jengo lililoporomoka na kwenda kuziuza na kwamba wakikamatwa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
‘MAGHOROFA YOTE DAR ES SALAAM SIYO SALAMA’
Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia, akizungumza jana na waandishi wa habari, alisema majengo mengi hususani maghorofa katika Jiji la Dar es Salaam siyo salama kwa kuishi.
Mbatia alisema majengo hayo siyo salama kutokana na kujengwa chini ya kiwango na kwamba kama kukitokea tetemeko la ardhi, majanga yanaweza kutokea kila wakati.
Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema kutokana na hali hiyo, serikali inatakiwa kuchukua maamuzi magumu kuwaondoa wananchi wanaoishi katika maghorofa na kufanya utafiti wa majengo hayo kubaini kama yana uimara unaotakiwa.
“Vifaa vya ujenzi TBS (Shirika la Viwango la Taifa) linapitisha tu, pia wapo watu wanaotoa vibali nao wanatoa vibali tu bila kufanya utafiti na kufuatilia ujenzi wa maghorofa, hii ni hatari katika nchi yetu,” alisema Mbatia.
Mbatia ambaye ana taaluma ya uhandisi alisema: “Yametokea matukio mengi ya maghorofa kuporomoka, lakini bado hatujajifunza na tukio hili lililotokea mfano likijitokeza jingine hili lililotokea litasahaulika.”
Alisema kuna haja ya kuwa na kitengo maalum cha kushughulikia majanga na wabunge katika mkutano ujao wa Bunge wanatakiwa kushinikiza suala hilo.
Naye Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali, alisema ghorofa pacha na lililoporomoka lililokuwa likijengwa na mkandarasi mmoja linatakiwa kubomolewa haraka ili lisije likasababisha janga jingine.
“Serikali ilibomoe haraka jengo hili na kama haitatekeleza tutajua kuna mkono wa rushwa, tunahitaji kuona nguvu ya John Magufuli (Waziri wa Ujenzi) kama masuala ya ujenzi wa majengo siyo kwenye ujenzi wa barabara tu,” alisema Machali.
Machali alisema kama jengo hilo halitaangushwa, watatangaza mgogoro na serikali.
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI KUTOA TAMKO
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye, alisema wizara yake itatoa tamko la serikali baada ya kazi ya kufukua kifusi cha ghorofa hilo lililoporomoka kukamilika.
Medeye alisema utata kuhusu kibali kilichotolewa kama kilikuwa cha kujenga ghorofa tisa au 16 litatolewa ufafanuzi.
KIKWETE ATEMBELEA WAJERUHI MUHIMBILI
Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete jana waliwatembelea majeruhi wa ajali ya jengo lililoporomoka hivi karibuni waliolazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Rais Kikwete aliyeambatana na mkewe, Salma na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadiki, alifika MNH majira ya asubuhi kwa ajili ya kuwajulia hali majeruhi hao.
Alitembelea wodi ya Sewahaji namba 17 walikolazwa majeruhi wawili, pamoja na Taasisi ya Mifupa (Moi) katika wodi binafsi ya wagonjwa walikolazwa wengine wawili.
Akizungumzia tukio hilo juzi, Kova alisema zoezi ya uokoaji liliendelea usiku kucha na miili hiyo imehifadhiwa MNH ilikowekwa kambi itakayosaidia watu kugundua miili ya ndugu zao.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment