ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 16, 2013

VIGOGO WIZARA YA ARDHI KORTINI KWA UBADHIRIFU

Simoni Lazaro (kushoto) akiwa na mtuhumiwa mwenzake, Gerald Mango.
Watuhumiwa hao wakiwa mahakamani.
Charles Kijuba akikwepa kamera mahakamani.
MAOFISA watatu waandamizi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi leo wameburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za ufujaji wa pesa za serikali zaidi ya milioni 200. Watuhumiwa hao ni Simon Lazaro ambaye alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Sera, Gerald Mango, Mkuu wa Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi , na Charles Kijuba, Kaimu Mhasibu Mkuu.
Watuhumiwa hao wamekana mashitaka na mahakama hiyo imesema kuwa dhamana iko wazi .

Picha na habari Haruni Sanchawa na Makongoro Oging.
GPL

No comments: