Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Charles Kenyela.
|
Watuhumiwa hao walikamatwa katika wiki ya kuelekea sikukuu ya Pasaka katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo, pia wamekuwa wakifanya uhalifu katika maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Charles Kenyela, alisema baadhi ya matukio ya wizi wanayofanya wahalifu hao ni pamoja na kukata vyavu za madirisha na kuiba simu kwa kutumia ndoano iliyofungwa kipande cha wavu wa chandarua.
Alisema baadhi ya waalifu hao, hutumia mbinu ya kukata makufuli na makomeo ya milango kwa kutumia mikasi maalumu na kufanikiwa kuingia ndani na kufanya vitendo vya uhalifu.“Jeshi la Polisi liliimarisha ulinzi na usalama katika mkoa wa Kinondoni kwa kufanya doria na misako katika maeneo yote na hatimaye tukafanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao, na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika,” alisema Kenyela.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa huo limefanikiwa kukamata silaha aina ya Shortgun mbili zenye namba, AB 44736 na 10883 pamoja na risasi 17 maeneo ya Kigogo baada ya wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.
Pia walifanikiwa kukamata bastola aina ya Glock 19 yenye namba LZB 642 na TZ CAR 98189 ikiwa na risasi 12 na ganda moja tupu maeneo ya Mabibo kufuatia msako mkali uliofanyika baada ya kutokea kwa tukio la wizi maeneo ya Msasani.
Kamanda Kenyela alisema, Bastola hiyo iliibiwa kwenye gari baada ya mmiliki kuingia benki ya DTB na kuiacha silaha yake ndani ya gari, ndipo wezi walifika na kuvunja kioo cha gari hilo na kuiiba pamoja na nyaraka mbalimbali.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment