ANGALIA LIVE NEWS
Friday, April 12, 2013
ZANZIBARI KUJITANGAZA KIMATAIFA
WIZARA ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, imesema itajiandaa kuona inatenga fedha kwa ajili ya kuandaa vipindi vya Utalii, vitavyoweza kurushwa katika idhaa za kimataifa.
Waziri wa Wizara hiyo Said Ali Mbarouk, aliyasema hayo jana wakati akijibu suala ala Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Nassor Salum Aljazira, aliyetaka kujua ni kwa nini Wizara hiyo inashindwa kuwa na vipindi vya utalii katika mashirika ya Habari ya kimataifa.
Akijibu suala hilo , Waziri huyo, alisema ni kweli suala ala kuutangaza utalii wa Zanzibar katika Mashirika ya Habari ya Kimataifa, ni jambo la msingi katika kukuza utalii lakini tatizo kubwa linalojitokeza ni suala la kuwapo kwa bajeti ndogo ndani ya Wizara hiyo.
Kutokana na ahali hiyo ni vyema Wajumbe wa Baraza hilo kuiona hali hiyo na kusaidia namna ya kulitatua katika abajeti yake ya mwaka huu kwa kuhakikisha mafungu ya vipindi hivyo yatapowekwa wayapitishe.
Akiendelea Waziri huyo, kujibu suala la msingi la Mwakilishi wa Muyuni Jaku Hashim Ayoub, alietaka kujua ni kwa kiasi gani vurugu zilizowahi kujitokeza hapa nchini zimeweza kusababisha hasara kwa watalii alisema ni kweli zilichangia kupunguza watalii kwani walifikia asilimia 2.5 ambayo ni sawa na watalii 3,721 kwa kipindi cha Januari hadi Novemba 2011.
Alisema kutokana na hali hiyo, kwa upande wa mapato yanaypkusanywa na Kamisheni ya Utalii kutokana na leseni za magari ya watalii na watembeza watalii hayakushuka ila athari zilionekana kutokea kwa Mamlaka ya ukusanyaji wa mapato ZRB ambapo hadi mwezi Mei 2012 yalifikia shilingi bilioni 8, sawa na asilimia 13, ikilinganishwa na Makusanyoya shilingi bilioni 10 kwa mwezi April 2012.
Hata hivyo Waziri huyo aliseka hali hiyo ilionekana kubadilika kuanzia mwezi Oktoba ambapo mapato hayo yalifikia asilimia 4.6 kwa kukusanya shilingi bilioni 12.2 na akufikia shilingi bilioni 12.8.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment