ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 12, 2013

MAPATO YA ZRB YAPOROMOKA

Serikali ya Zanzibar imekiri makusanyo yake kuporomoka na makusanyo ya Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) mwezi wa Mei 2012 yameanguka kufikia fedha za Tanzania shilingi 8 bilioni sawa na asilimi 23% ukilinganisha na makusanyo ya shilingi 10 bilioni kwa mwezi Apil 2012 .

Kwa upande wa mwezi wa Octoba 2012 takwimu hizo zinaonesha kuwa makusanyo ya ZRB yameongezeka kwa asilimia 4.6% kutokana tsh 12.2 bilioni na kufikia tsh 12.8 bilioni.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na michezo Saidi Ali Mbarouk alisema hayo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi wakati akijibu suli la msingi liloulizwa na mwakilishi wa jimbo la Muyuni Jaku Hashim huko Mbweni nje kidogo ya mji ya Zanzibar.

Mbarouk alisema wakati wa vurugu kulikuwepo usitishwaji wa safari kwa wageni wakihofia usalama wao kwa kuwa misafara ya kitalii inaratibiwa na tasisi binafsi za ndani na nje ya nchi imekuwa vigumu kupata takwimu sahihi ya wageni waliositisha safai zao.

Hata hivyo kwa kulinganisha vipindi vya miezi inavyofuatana takwim zinaonesha kuwa watalii walipungua kwa asilimia 2.5 ambayo ni sawa na watalii 3,721 kwa kipindi cha January hadi Novemba 2011.

Serikali kupitia tasisi zake inaendelea kutoa elimu kwa vijana na wananchi kwa ujumla kutokana na madhara yatokanayo na vurugu na uvunjifu wa amani kwa ustawi wan chi.

Wizara kupitia kamati za utalii za wilaya ipo katika hatua za kukamilisha maandalizi ya semina na makongamano katika vijiji na ili kuelimisha wananchi juu ya athari za vurugu na umuhimu wa kudumisha amani na utulivu nchin kwa maendeleo ya sekta ya utalii na nchi kwa ujumla.

No comments: