Wednesday, May 15, 2013

2013 GLOBAL DIASPORA FORUM YAFANYIKA WASHINGTON DC- May 13-14

Global Diaspora Forum ambayo kila mwaka uwakutanisha Wawakilishi ,Viongozi mbalimbali wa Diaspora kutoka nchi mbali mbali ilifanyika Washington DC May 13 na 14.  Forum hii huandaliwa kila mwaka na USAID , US Department of state na International Diaspora  Engagement Alliance . Mwaka huu Forum hii ilikusanya washiriki wapatao 510. Lengo kubwa la Forum hii ni kujadili mambo mbalimbali yanayo wahusu Diaspora. 
(Pichani mkuu wa USAID Dr.Rajiv Shah Akifungua Rasmi 2013 Global Diaspora Forum kwenye makao makuu ya USAID , jijini Washingon, DC (May 13))
Acting Special Representative for Global Partnerships Ititiatives, U.S Department of States Mr. Thomas Debas, akifungua rasmi siku ya pili ya Global Diaspora Forum ambayo iliendelea  US Department of States Headquarters. (May 14, 2013)
Rais wa Jumuiya ya Watanzania Washington DC, Maryland and Virginia Bwana Iddi Sandaly (kulia) akiwa na Bwana Ben Kazora (kushoto) ambae ni President wa Eastern African Countries Diaspora Council  ni watanzania wawili ambao walikuwa wakiwakilisha. Katikati ni Mr.James Ihedigbo Mchezaji wa kulipwa wa Mabingwa wa  Football ya kimarekani (NFL) Baltimore Ravens ambae pia ni mwanaDiaspora.
Mkutano ukiendelea
Rais wa Jumuiya Iddi Sandaly katika picha wakati akiwa kwenye mkutano huo/
Dada Lisa Kibede Actress, Supermodel na Designer ambae ni mzaliwa wa Ethopia akichangia machache.
   Bwana Meb Keflezighi ambae ni Raia wa Marekani na Eritriea ambaye ni mwanariadha wa kimataifa na mshindi wa Olympic silver medal akiwakilisha USA mwaka 2004  akiwa na Michelle Kwan ambae ni Figure Skater, pia ni mwanaDiaspora mwenye asili ya china na aliwahi kushinda medali mbili za Olympic na kuwa bingwa wa dunia mara nne.
Billionea Bwana Hamdi Hulukaya , CEO na Mmiliki wa Kampuni ya Chobani Yogurt, akielezea jinsi gani alivyonufaika kwa kuja USA .
kwa picha zaidi bofya read more

Hall Ambalo forum ya siku ya Pili ilifanyika- US Department of State Headquarters

No comments: