Thursday, May 23, 2013

ACHA ULIMBUKENI, SI LAZIMA ‘KUDUU’!-2


NDUGU zangu, wiki iliyopita nilianza kuzungumzia ulimbukeni walionao baadhi ya watu kutokana na kuweka mbele suala la kufanya mapenzi hata katika mzingira ambayo hayaruhusu.

Nilizungumzia ishu ya wale ambao wako katika uchumba lakini wanalazimishana kukutana kimwili huku ikionekana kama jambo la lazima. Yaani mwanaume anadhani akishaanzisha uhusiano na msichana basi amejikatia tiketi ya kupewa mapenzi hata kabla ya kuingia kwenye ndoa.
Mbaya zaidi baadhi ya wanaume wanalazimisha kabisa na wakikataliwa huona kama vile hawapendwi, hivyo hufanya maamuzi ambayo mara nyingi humuathri msichana ambaye ameingia kwenye uhusiano lakini akawa na msimamo wa kutotaka suala la mapenzi mpaka watakapoingia kwenye ndoa.
Wapo mabinti ambao wamejikuta wakisalitiwa sana na wapenzi wao kutokana na misimamo yao kwa wachumba zao ya kujitunza mpaka watakapoingia kwenye ndoa. Wenyewe wanafanya hivyo kulinda heshima yao lakini pia kukwepa ile mitego ya wanaume wanaotangaza ndoa kwa ajili ya ‘kumega’ mabinti kisha kuwatema.
Achilia mbali hao ambao wamekuwa wakisalitiwa, wapo ambao wametoswa kabisa. Mwanaume anaingia kwenye uhusiano, baada ya muda mfupi anaomba mapenzi na anaambiwa avute subira waje wafurahie tendo hilo baada ya ndoa lakini yeye anaona anacheleweshwa na anaamua kuingia mitini, waliofanya hivyo wapo wengi huko mtaani.
Ndiyo maana nikasema, tuache ulimbukeni wa kudhani kufanya ngono ni jambo la lazima. Kama kweli tunaanzisha uhusiano kwa nia njema ya kuelekea kwenye ndoa, basi lazima tuwe na subira. Tusilazimishe mambo ambayo huenda yanawakwaza wapenzi wetu.
Hapu juu nimegusia zaidi wanaume ambao ndiyo wanaoonekana kulazimisha penzi lakini sasa, kuna wanawake ambao na hawapendi kuingia kwenye uchumba ‘siriasi’ kabla ya kukutana kimwili na wanaume ambao wametokea kuwapenda.
Ukiwauliza utagundua wengi wanaangukia kwenye kisa hiki kifuatacho. Msichana mmoja alipata mwanaume baa, wakaanza uhusiano wao lakini ndani ya kipindi cha miezi miwili yule mwanaume akamwambia mpenzi wake kuwa, lengo lake ni kuoana lakini kuhusu kukutana kimwili ni mpaka watakapofunga ndoa.
Yule msichana akakubaliana na wazo la mpenzi wake lakini akili yake ikawa inamshangaa sana yule mwanaume. Akawa anajiuliza inakuwaje mwanaume kama yule ambaye wamekutana baa aweze kutoa uamuzi huo? Kumbe bwana mwanaume alikuwa na lake jambo.
Basi siku zikaenda, ndoa ikafungwa vizuri huku mwanamke akijua amepata mwanaume kumbe…!
Baada ya kuingia kwenye ndoa ndipo yule msichana alipogundua kuwa, kilichokuwa kinamfanya yule mwanaume akatae kukutana naye kimwili kabla ya ndoa ni maumbile yake makubwa.
Alijua mwanamke akishauona uume wake asingekubali kuolewa naye. Hata baada ya kuingia katika ndoa na mwanaume yule msichana yule hakuweza kuvumila kwani alipoona hali halisi alilazimika kuomba talaka.
Tunajifunza nini katika kisa hiki? Sina haja ya kufafanua zaidi lakini umeona kwamba kuna sababu ya angalau kumjua kiduchu nje na ndani mchumba wako ili hata pale utakapokuwa unafanya uamuzi wa kuolewa naye una uhakika kuwa atakufaa. Hata hivyo, nazidi kusisitiza, siyo lazima kuduu. Kumbuka unapokutana kwa mara ya kwanza faragha na mtu uliyempenda mkiwa ndani ya ndoa kuna raha yake.

GPL

No comments: