Thursday, May 23, 2013

BAADA YA KUSUSA KULA SIKU2 SASA AFANDE MAMBO SAAFII

BAADA ya kususa kula kwa siku mbili mkali wa ghani ‘Rymes’ nchini msanii Selemani Msindi ‘Afande Sele’ amesema ameanza kula baada ya kushusha fundo lake la timu ya Simba kulala 2-0 na watani wao wa jadi Yanga.

Afande Sele ameweka wazi ilibidi agome kula kutokana na mke wake ambaye ni shabiki wa Mabingwa wa Ligi Kuu Bara Yanga.Msindi aligoma kula siku moja baada ya mechi hiyo ya watani wa jadi Simba na Yanga iliyopigwa Mei 18 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Akizungumza kwa njia ya simu na Bongoweekend alisema kwamba uchungu ulizidi baada ya mkewake mama Tunda alizidisha utani nyumbani kwake hivyo akaona bora asuse kula kwa siku mbili lakini sasa maisha yanaendelea ,huku akimalizia kwa kicheko.

No comments: