Thursday, May 23, 2013

SHILOLE & FM ACADEMIA KUSINDIKIZA REDDS MISS KURASINI

BENDI ya muziki wa dansi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ na mwanamuziki wa kike anayetamba katika miondoko ya muziki wa mduara Shilole wametajwa kutoa burudani katika shindano la kumsaka Redds Miss Kurasini 2013. 

Akiuzngumza na jana Mratibu wa shindano hilo Yasson Mashaka alisema kuwa hizo ndizo burudani zitakazo wasindikiza warembo hao watakaocvhuana kuwania taji la kituo hicho shindano lililopangwa kufanyika Mei 24 katika ukumbi wa Equator Grill Mtoni kwa Aziz Ally.

Jumla ya washiriki 12 watapanda jukwaani katika kuwania taji hilo ambapo pia wako katika hatua za mwisho za mazoezi yanayoendelea katika ukumbi huo chini ya mwalimu wao Lupatu ambaye aliwahi kushiriki shindano la kanda la Miss Kinondoni 2012 akitokea Kanda ya Kinondoni.

Yasson anawataja washiriki hao na umri kwenye mabano kuwa ni Stella Muganyizi (19), Bandio Byela (20), Violet Mushi (20), Svetlana Nyameyo (20), Jacqueline Ngoma (19),Catherine Manyama (21), Darline Mmary (20), Mainda Abdi (21), Maryclara John (19), Eliza John (19), Shumesa (20) na Latifa Suleiman (20).

Taji la Redd’s Miss Kurasini linashikiliwa na Flaviana Maeda ambaye alibahatika kushiriki katika fainal za Miss Tanzania 2012. 

Shindano hili limedhaminiwa na Redd’s Premium Cold , PJ Amusement, Jambo Leo, Dodoma Wine, Naeem Classic, Kitwe General Suppliers,Father Kidevu Blog, House ofa Nails and Eye browes na Clouds FM.

No comments: