Tuesday, May 14, 2013

WANAFUNZI WA SHULE YA SECONDARI MANZESE ZAIDI YA 30 WAANGUKA HOVYO HOVYO

Wanafunzi wa shule ya secondari manzese zaidi ya 30 muda huu wanaanguka hovyo hovyo na kusema a mane no yasiyoeleweka kutokana na kinachohisiwa kuna nguvu za Giza zimetanda shuleni hapo huku wakijibamiza kwenye miti:
Tukio hilo limetokea kuanzia saa nne asubuhi ambapo alianza mwanafunzi mmoja kupiga kelele na kuanguka wakati wakiendelea na masomo ambapo alitolewa nje ya darasa lakini cha kushangaza waliendelea
kuanguka wengine wengi huku wakipiga kelele na kupigana kama vichaa.
Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese aliyeanguka na kuweweseka.Mpaka sasa haijafahamika chanzo cha wanafunzi wa shule hiyo kukimbia ovyo,kuanguka na kuweweseka.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese iliyopo Manzese Uzuri, jijini Dar es Salaam wamevamiwa na mashetani na kuanguka hovyo darasani huku wakipiga kelele na kuongea maneno yasiyoeleweka na kusababisha hofu kutanda maeneo hayo.
Picha:Zainab Chondo wa ITV

1 comment:

Anonymous said...

haya tena vinyamkera vinawaka uchana kweupe wanawangia watoto maskini za mungu,sasa waheshimiwa na wana dini wanasemaje?

wanataka kafara za damu ikifika mwezi wa nane chunguzeni sana mtaona maajabu kama haya mengi tu watu kupoteza maisha kwenye ajali etc

wanga ndo siku zao za kunywa na kula damu nakuabiyeni kweli fanyeni uchunguzi huu mtaona

yule mdada wa kiislamu aliyekwenda benki kuchukua pesa akauliwa vibaya mchana kweupe

na hawa wanga na vinyamkera si wa kuchezea wako local na pia global ambao maraisi wa nchi za ulimwengu wa kwanza wanajiunga nao someni