Advertisements

Tuesday, May 7, 2013

Chadema wamchangia mtoto upasuaji wa moyo

"Viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro baada ya Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema kumtambulisha jukwaani mama mzazi wa mtoto huyo, Selina Peter aliyefika mkutanoni hapo kuomba msaada wa Dola 2,700 za Marekani kwa wasamaria kufanikisha matibabu ya mwanaye."

Arusha. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilaya ya Arusha, kimetoa mchango wa zaidi ya Sh1.3 milioni kusaidia gharama za operesheni ya moyo kuokoa maisha ya mtoto, Beatrice Shemtibuko (1.7), anayetakiwa kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Fedha hizo zilichangwa na wafuasi wa chama hicho wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro baada ya Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema kumtambulisha jukwaani mama mzazi wa mtoto huyo, Selina Peter aliyefika mkutanoni hapo kuomba msaada wa Dola 2,700 za Marekani kwa wasamaria kufanikisha matibabu ya mwanaye.

Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha, Martin Sarungi alimkabidhi mama wa mtoto huyo hundi ya Sh 1.39 milioni alizosema ni mchango wa wananchi .

Wenye nia ya kuchangia matibabu ya mtoto huyo wanaweza kufanya hivyo kupitia mtandao namba za simu 0757386623, 0655386623 akaunti namba 0142030004968 Benki ya NBC Ltd.
Mwananchi

No comments: