ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 7, 2013

SARATANI INAEPUKIKA, ZINGATIA HAYA!

Nyama
Maji
Hiyo ni nukuu kutokana Chama Cha Wenye Saratani cha nchini Marekani, nukuu ambayo inatakiwa kuchukuliwa kwa uzito mkubwa na kutambua kwamba jukumu la kujiepusha na magonjwa ya saratani linaanza na ‘wewe’.

Zifuatazo ni njia za kuzuia uwezekano wa mtu kupatwa na saratani iwapo atazingatia haya:

KUWA NA VITAMIN D
Hakikisha unaota jua ili kupata kiwango cha kutosha cha Vitamin D mwilini. Kama huna nafasi ya kupata mwanga wa jua, kula vidonge vya Vitamin D3. Imethibitika na wanasayansi kuwa mwili ukiwa na Vitamin D ya kutosha, unajiepusha na uwezekano wa kupatwa na magonjwa ya saratani.

ULAJI WA PROTINI ULIOKITHIRI
Baadhi yetu tuna kiwango kingi cha protini mwilini kutokana na kupenda sana kula vyakula kama vile nyama. Tunashauriwa kula nyama au vyakula vingine vinavyoongeza protini kwa siku kiwango kisizidi gramu 100, inaruhusiwa kuzidisha kiwango hicho kwa kina mama waja wazito na watu wenye kufanya mazoezi ya kukimbia kwa umbali mrefu.
VYOMBO VYA KUPIKIA
Hakikisha unatumia vyombo vya kupikia ambavyo vimeoshwa kwa kutumia sabuni ya kawaida pamoja na maji safi. Usipende kuosha vyombo vyako kwa kutumia dawa zenye kemikali nyingi…baadhi ya kemikali huleta saratani.

BIDHAA ZA NGOZI
Kuna aina nyingi sana za bidhaa za ngozi, lakini baadhi ya bidhaa hizo, kama vile losheni, krimu, mafuta, n.k zimetengenezwa kutokana na kemikali ambazo zinaaminika kusababisha saratani. Unashauriwa kujiepusha na bidhaa hizo na badala yake tumia bidhaa zilizotengenezwa kutokana na mimea au matunda asilia.

MAJI SALAMA
Hakikisha unakunywa maji mengi kila siku yaliyo safi na salama, yaliyohifadhiwa katika vyombo visafi na kuwekewa dawa ya kusafisha maji ambayo inakubalika.

VYAKULA VYA MADAWA
Jiepushe na ulaji wa vyakula, kama vile mboga, matunda na mimea mingine iliyooteshwa na kustawishwa kwa kutumia madawa ya kunenepesha mimea hiyo (GMO). Badala yake, kula vyakula vilivyolimwa na kustawisha kwa kutumia udongo na mbolea asilia (Organic Food).

VYAKULA VYA MAKOPO
Epuka ulaji wa vyakula vilivyotengenezwa na kuhifadhiwa kwenye makopo. Kemikali zinazotumika kutengenezea makopo hayo ili yaweze kuhifadhi chakula na kikae kwa muda mrefu zinadaiwa kusababisha kansa. Ili kuwa salama, jiepushe na ulaji wa vyakula vyote vya kwenye makopo.

ZINGATIA
Mwili uliumbwa ujikinge wenyewe pale unapovamiwa na adui ambaye ni ‘magonjwa’. Ili mwili uweze kufanya kazi yake hiyo, upe uwezo na uwezo wake uko kwenye vyakula, hasa vyakula vya mboga, kama vile nyanya, vitunguu, kabichi, brokoli, matunda kama vile nanasi, embe, stafeli, mafenesi, na mengine mengi. Ukiwa na tabia ya kula matunda na mboga mara kwa mara, una uhakika wa kinga imara ya mwili, si kwa saratani tu, bali kwa magonjwa yote hatari.
GPL

No comments: