Katika pita pita zetu tumekutana na kijana aitwaye Saleh Abdul anayedai kuwa ni mdogo wake na Diamond Platnumz. Saleh anadai yeye na Diamond wanachangia baba lakini jitihada zake za kuwa karibu na kaka yake zimekuwa zikigonga mwamba kwakuwa hitmaker huyo anadai kumkana.
“Mimi ni mtu ambaye nina kipaji cha kuimba lakini najikuta kwamba naambulia patupu yaani kukosa msaada wowote, nikimwendea kaka yangu Diamond anashindwa kunielewa, hataki kunisaidia, halafu wakati mwingine ananikana kabisa kwamba mimi sio mdogo wake,” amesema Saleh kwa uchungu.
Tunafanya jitihada kumtafuta Diamond athibitishe kama kweli Saleh ni mdogo wake.Jina halisi la Diamond ni Naseeb Abdul.
Bongo5
3 comments:
Aah kwani ukiwa ndugu yake huwezi kutoka kivyako mpaka upitie kwake? Wabongo wanaboa sana kwakupenda dezo. Ivi Diamond angekua bado muuza mitumba ungemtafuta kiivyo? Tafuta kivyako sio kupitia migongo ya watu wengine.
Aah kwani ukiwa ndugu yake huwezi kutoka kivyako mpaka upitie kwake? Wabongo wanaboa sana kwakupenda dezo. Ivi Diamond angekua bado muuza mitumba ungemtafuta kiivyo? Tafuta kivyako sio kupitia migongo ya watu wengine.
You don't need a DNA test to prove you case. Wewe ni mgogo wake na Diamond kabisa. Sasa dogo, migogoro ya kifamilia inajadiliwa nyumbani. Ungetafuta watu wazima wakakusaidia kukaa na kaka yako kujadili malalamiko yako. Sidhani kama kukimbilia kwenye vyombo vya habari unaweza kupata msaada unaouhitaji, badala yake inakuwa siyo tu kumdhalilisha kaka yako, bali familia nzima. Mimi ningekushauri usome kwanza. Muziki upo tu na kipaji chako hakipotei. Pia ni vizuri uelewe kuwa hakuna sheria inayomtaka kaka kumsaidia mdogo wake. Kusaidiwa au kutosaidiwa kunategemea jinsi mlivyolelewa.
Post a Comment