HIVI, hujawahi kusikia mtu akisema: “Ah! Bwana simuwezi yule mwanamke ni kiburi sana...ni mkorofi sana. Sitawezana naye. Hata kama nampenda lakini tabia zake mimi siziwezi!”
Mwanaume mwenye kutoa kauli kama hii anaweza kuwa yupo kwenye hatua za mwisho za kuelekea kwenye ndoa na mwanamke wake au tayari wamo ndani ya ndoa.
Inawezekana kabisa kuwa ni kweli mwanamke wake ni mkorofi lakini amejaa moyoni mwake kwa mapenzi tele tena ya dhati. Je, anawaza sawa? Tiba ni kumuacha? Ana mazuri mengi, lakini ni mkorofi tu. Amuache?
Hapa kwenye kutoa maamuzi ndipo kulipozalisha mada hii. Kiukweli, hili ni tatizo kubwa sana kwa wanaume wengi. Kwa kawaida hulka ya mwanaume ni kuheshimiwa, kunyenyekewa na kusikilizwa.
Hivi ndivyo walivyoumbwa, ndiyo maana inapotokea mwanamke akashindwa kumheshimu mwanaume, hasira huweza kupanda na kusababisha kumuangushia kipigo. Kimsingi ni tatizo ambalo kama lisipo-dhibitiwa mapema, linaweza kusababisha mgogoro katika familia.
Hapa kuna umuhimu wa kujifunza juu ya jambo hili lenye umuhimu mkubwa katika maisha yetu. Hebu tuone sasa.
KWA NINI WANAUME?
Kama nilivyoeleza hapo juu, hulka ya mwanaume ni kusikilizwa, kupewa nafasi ya kwanza na kumuongoza mwanamke wake. Kwa msingi huo inapotokea ametoa agizo fulani au wapo kwenye mazungumzo na mwenzi wake, halafu akajaribu kumweleza mpenzi wake kitu fulani, akampinga ndipo tatizo linapoanzia.
Mwanaume anajiamini, anaamini mawazo yake, lakini pia anapenda kutoa maelekezo kwa njia bora na ya kirafiki. Kwa tabia ya wanawake ninaowazungumzia hapa, hata kama mwanaume wake atazungumza kwa lugha nzuri kiasi gani, kama hataki ataleta jeuri huku akiwa hana pointi za kushibisha msimamo wake.
KIBURI/DHARAU
Ni hali ya kukiuka, kukataa au kubisha bila sababu za msingi. Mwanamke huyu ni kidomodomo, muongeaji sana na hataki kuelekezwa. Anajiamini yupo sahihi kwa kila hatua na mbishi kupitiliza.
Yote haya kwa pamoja, yakifanywa kwa mwanaume anayejua haki na wajibu wake, ndipo msuguano unapoanzia.
NI SABABU YA KUACHANA?
Yupo jamaa mmoja alinitumia meseji akisema: “Brother Shaluwa mimi nimechoshwa kabisa na tabia ya mpenzi wangu. Yaani ni kiburi kupindukia, kila ninachomwambia, anapingana na mimi. Kiukweli nimemchoka na ninataka kuachana naye moja kwa moja. Nimechoka sasa. Je, wewe unaonaje?”
Umeona maneno hayo? Je, unadhani yupo sawa? Kiukweli hayupo sawa. Kwa kawaida, kuna kasoro ambazo tunaziita ndogondogo na nyingine kubwa.
Wakati wa kuchagua mwenzi wa kuingia naye kwenye ndoa ni muhimu kukagua kasoro za mwenzako. Kuna nyingine zinavumilika na nyingine ni kubwa. Kwa bahati mbaya kuna wengine hadi wanaingia kwenye ndoa wanakuwa bado hawajajua kasoro za wenzao, mara anagundua kwamba mke wake ana kiburi na jeuri – siyo sababu ya kumuacha!
Rafiki zangu, kuna kitu cha kufanya zaidi ya kuachana. Hebu tuendelee kuona.
UPO UPANDE UPI?
Je, wewe unasumbuliwa na mwanamke mkorofi? Unaishi naye au ni mchumba wako? Rafiki yangu, msingi mkubwa unaoweza kubeba penzi lenu wakati unatafuta dawa ya ukorofi wake ni penzi la kweli moyoni mwako.
Kwanza umpende, utambue thamani yake, uuchukulie udhaifu wake kama sehemu ya mapenzi yako, halafu tafuta tiba ya tatizo lake. Je, mpenzi wako yupo upande upi?
Unajua kuna wanawake wengine ni wakorofi, lakini ukifuatilia sana ukorofi wao una maana. Unasaidia kwenye maeneo fulani. Si kila kinachozungumzwa na mwanaume kipo sahihi. Mwanaume anatakiwa kukubali kupewa mawazo na mwanamke wake. Tatizo lililopo ni namna mwenzi wake anavyowasilisha hoja yake kwa mwanaume wake.
Usiamini kila kinachotoka kinywani mwako kipo sawasawa, wakati mwingine unaweza kukosea na mwenzi wako akataka kukushauri. Jambo kubwa hapa ni namna gani basi, anavyoweza kuwasilisha hisia zake.
Mwanamke mwenye busara hana maneno mengi, huomba samahani kwanza, kisha kuanza kumweleza mwenzake anavyojisikia taratibu na kwa hoja. Si kuropoka. Si kejeli wala jeuri. Atajenga hoja yake kikamilifu kwa kutumia mifano na maneno yenye staha.
JIONE MWENYE JUKUMU
Nilitangulia kusema, ikiwa umeshamchunguza mwanamke wako vya kutosha na kufikia hatua ya kuingia naye katika ndoa, yupo moyoni mwako. Bila shaka utakuwa umeridhishwa na tabia zake zote.
Inawezekana huo ujeuri au ukorofi mwanzoni hakuwa nao na sasa unaona ni tabia mpya usiyoipenda na unatamani kuachana naye au kutoka kwenye ndoa (kwa wenye ndoa).
Kikubwa hapa unatakiwa kutambua kuwa mwanamke wako ana tabia hiyo, halafu pili ujue kuwa jukumu la kukabiliana na tabia hiyo lipo mikononi mwako. Hii itakuwa hatua nzuri ya kuelekea kwenye mafanikio.
Mada bado inaendelea marafiki zangu na kuna mengi zaidi ya kujifunza. Kutokana na nafasi yangu, nalazimika kuachia hapa leo, wiki ijayo tutaendelea, USIKOSE!

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia Magazeti ya Global Publishers. Ameandika Vitabu vya True Love, Let’s Talk About Love na All About Love vilivyopo mitaani.
No comments:
Post a Comment