ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 13, 2013

KUNA MTANZANIA YUPO CHUMBA CHA WAGONJWA MAHUTUTI, HOLY CROSS HOSPITAL, SILVER SPRING, MD

Kuna Mtanzania anaitwa Martin Ngireu yupo Holy Cross Hospital iliyopo Silver Spring, Maryland- USA yupo chumba cha wagonjwa mahututi tangu May 3, 2013 baada ya kuanguka kazini na hana ndugu yeyote hapa DMV yupo chumba # CCU2 Ghorofa ya 7.

Hali ya mgonjwa sio nzuri  tunaomba kama kuna ndugu yeyote au mtu yeyote anayemfahamu afike Holy Cross Hospital. Katika kuongea na mhudumu wa hospitali hiyo amesema kwamba kuna Watanzania wanaoishi California aliwataja kwa jina moja moja Biva, Elizabeth na Oscar pia Vijimambo ilipata simu toka kwa Upendo anayeishi Canada akisema huyo mgonjwa ni baba yake mdogo. Upendo alishawahi kuishi hapa DMV miaka ya nyuma.

Mhudumu huyo aliendelea kwa kusema kwamba uongozi hospitalini hapo umeiandikia barua Ubalozi wa Marekani Tanzania kuhusu kupatiwa VISA kwa ndugu wa karibu na mgonjwa ili aweze kuja nchini Marekani.

Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Idd Sandaly ambae alikuwepo Hospitalini hapo Jana Jumapili, amewaomba Watanzania hapa DMV wamtembelee mgonjwa na Watanzania wote wazidi kumuombea aweze kupata nafuu.

7 comments:

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous said...

Jamani Watanzania wenzangu please ukipata ajira kuna section ya EMERGENCY CONTACT please take that very serious na umweke ndugu au rafiki wa karibu hapa Marekani au popote pale alipo ukiacha blank siku emergency ikitokea inakuwa tabu sana kwa watu kukusaidia na update kama ulimwandika mumeo au mkeo na huko naye tena hatujui lini that EMERGENCY contact info simu email whatever you can put will come handy. Tunamwombea wana ndugu wapatikane jamani this is soo sad.

Anonymous said...

unajua wewe kama unataka kusaidia saidia ila usijifanye unajua kwa kutoa ushauri mimi binafsi niliweka emergency contact na jamaa alipopigiwa alikana kwamba hanijui sasa sioni umuhimu kwa hilo.

Anonymous said...

Ni muhimu sana kuweka contact. Unapewa nafasi tatu za kuweka majina. Pole yamekutokea wewe wa juu. Please people put your emergency contact information when asked.

Anonymous said...

wewe anonymous unayesema kuwa uliyemweka kakukana then you put the wrong person au uliyemweka alikuwa anaogopa kwa sababu ya issue zake binafsi maana unapopigiwa simu kuhusu rafiki au ndugu unayempenda utataka kujua kulikoni hapa tuko Marekani hata kama nataka kusaidia sintoruhusiwa na hospitali kufanya maamuzi yeyote. Ndiyo maana tunatafuta ndugu zake wakijitokeza then sisi wa mbali kama watanzania tutasaidia. Kama upo bongo huku majuu mtu anapokuwa mahututi hajitambui ni ngugu zake wa damu tuu wanaweza kuongea na hospitali na kutoa msaada wa kuamua matibabu gani afanyiwe na kuna document za kusign, so please huo ulikuwa ni ushauri mzuri wa kukumbushana mambo muhimu kwani tunaishi kwenye nchi zenye sheria tofauti na utamaduni wetu wa kibongo. Please ndugu zangu mlio ughaibuni angalia emergency contact zako popote ukipo na hakikisha zipo sahihi whether upo college au kikazi. Mungu amsaidie mgonjwa aweze kupona.

Anonymous said...

Pole wewe wa hapo juu. Kabla ya kumweka mtu mfahamishe kuwa unamweka pia pata watu watatu kama mesmaji hapo juu. Kumbuka miili yetu ni ya kuazima hivyo wakati mwingine inahitaji mtetezi wa karibu!

Maombi ya nguvu kwa mgonjwa!!

Anonymous said...

kuweka contact number ni muhimu kuna wengi zimewasaidia, hakuna haja ya kueleza nini na nani imefanya kazi au kuendeleza malumbano contact ni muhimu, walioweka kipengele hicho wameona umuhimu wake kuwepo, tusipotoshane kwa fikra zisizofanya kazi