Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi akitoa kauli ya Serikali Bungeni kuhusu vurugu zilizotokea Mkoani Mtwara.
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akiahirisha Bunge kutokana na vurugu zilizotokea Mkoani Mtwara
Waziri wa Nchi ofis ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Merry Nagu akiomba kutengua kanuni ya Bunge Na. 38 ili kuruhusu suala la vurugu za Mtwara kujadiliwa Bungeni.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akizungumza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Frederick Werema pamoja na baadhi ya Mawaziri ndani ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirishwa kwa kikao cha Bunge .
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo akizungumza na baadhi ya Mawaziri na Wabunge ndani ya ukumbi wa Bunge mara baada ya Spika wa Bunge kuahirisha bunge
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Emmanuel Nchimbi (Kushoto) akizungumza na mbunge wa Kinondoni Mhe. Iddi Azzan nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya bunge kuahirishwa.
Wabunge wa Viti Maalumu wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge baada ya Spika kuahirisha Bunge. Kutoka kushoto ni Mhe. Lucy Owenya(CHADEMA), Katikati Mhe. Mkiwa Kimwanga(CUF) na kulia ni Mhe. Dkt. Merry Mwanjelwa(CCM).
Naibu Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Pereira Ame Silima (Katikati), Naibu wa Viwanda na Biashara Mhe. Greygory Teu (kushoto) na mbunge wa Kilosa Mhe. Mustafa Mkullo wakizungumza nje ya ukumbi wa Bunge.
Kundi la Waandishi wa Habari wanaoripoti habari za Bunge wakitoka ndani ya ukumbi huo mara baada ya Spika wa Bunge kuahirisha kikao cha Bunge.
PICHA NA ZAWADI MSALLA-MAELEZO DODOMA
2 comments:
jamani kuna haja gani ya kuwa na wabunge wote hoa na bado wanashindwa kutatua swala moja kwa hiyo wanahairisha lakini wamelipwa tayari na kesho wakirudi ni utumbo uleule watasema....wabunge wengi kazi ni sifuri ....ndiyo maana hatuendelei..lazima mabadiliko ya tokee this is too much now...vitambi tu na unene
Bunge letu ni kichwa cha mwendawazimu
Post a Comment