Miss Universe Tanzania Winfrida Dominique akitoa somo la madhara ya madawa ya kulevya kwa wanafunzi wa kidato cha tano wa shule ya sekondari ya Azania jijini. Winfrida alitoa somo hilo kwa dakika 40 kwa kushirikiana na Dk Johaness Mafwiri wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili na taasisi ya New Hope Tanzania Limited (NEHOTA) ambayo inajishughulisha na kazi ya utoaji ushari nasaha kwa watumiaji wa madawa ya kulevya na mambo mengine. Picha Sufianimafoto
Miss Universe Tanzania, Winfrida Dominique amewataka vijana nchini kutothubutu kutumia madawa ya kulevya kwani wao ndiyo tegemeo la taifa hili.
Winfrida alisema hayo wakati akitoa mafundisho kuhusiana na madhara ya madawa ya kulevya kwa wanafunzi wa kidato cha tano wa shule ya sekondari ya Azania jana.
Mrembo huyo alisema kuwa madhara ya madawa ya kulevya ni makubwa sana hapa nchini hasa kwa vijana na yeye kama mmoja wa vijana, atatumia taji lake kutoa elimu kuhusiana na madhara ya madawa hayo.
Alisema kuwa amejionea mwenyewe jinsi vijana wanavyoathirika na utumiaji wa madawa ya kulevya na taifa kupoteza nguvu kazi muhimu pamoja na matatizo ya ajira nchini.
“Nitatumia taji langu kutoa elimi mbali mbali ili kuwarejesha baadhi ya vijana waliopotea kurejea katika njia iliyonyoofu na kufanya kazi nyingine hata kwa kujiajiri, nitaendelea kutoa elimu hii kwa wanafunzi wengi zaidi, ” alisema Winfrida.
Mrembo huyo alitoa mafunzo hayo kwa kushirikiana na Dk Johaness Mafwiri wa taasisi ya New Hope Tanzania Limited (NEHOTA) ambayo inajishughulisha na kazi ya utoaji ushari nasaha kwa watumiaji wa madawa ya kulevya na mambo mengine.
Mbali ya Winfrida, Dk Mafwiri naye alitoa mada iliyohusiana na madawa ya kulevya na ulevi wa kupindukia ambao ni hatari kwa vijana na kwa upande wa elimu pia.
“Madawa ya kulevya yapo ya aina nyingi, lakini maarufu ni Cocaine na Heroine, lakini bhangi na ulivi kupindukia ni moja ya madawa ya kulevya na yanatofautiana kwa upande wa madhara yake, si vizuri kwa vijana na hata kwa jamii kiujumla,” alisema Mafwiri.
No comments:
Post a Comment