ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 24, 2013

Obama ‘afunga’ hoteli katikati ya jiji

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe 
Dar es Salaam. Wakati Rais wa Marekani, Barrack Obama akitarajiwa kuwasili na msafara wa watu 700, baadhi ya hoteli zenye hadhi ya nyota tano jijini Dar es Salaam zimeanza kusitisha kupokea wageni kutokana na ujio huo.
Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani ilisema Rais huyo, anatarajiwa kuwasili nchini Julai Mosi kwa ajili ya ziara ya siku tatu hadi Julai 3 mwaka huu ili kuimarisha uhusiano baina ya nchi hiyo pamoja na nchi za Afrika. Msafara huo utajumuisha watu mbalimbali wakiwamo wafanyabiashara.
Akizungumzia ziara hiyo jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema tayari timu ya kwanza imewasili nchini kwa ajili ya maandalizi mbalimbali.
“Ni ujio mkubwa na atakapokuwa nchini atazungumzia masuala mengi ikiwamo namna ya kuiwezesha Afrika kuwa na umeme wa kutosha kwa sababu ukiwa nao maendeleo yanakuwa mazuri,”alisema Membe.
Hoteli zasitisha upokeaji wageni
Gazeti hili lilifanya uchunguzi katika hoteli mbalimbali zenye hadhi ya nyota tano ambazo mara nyingi viongozi wakuu wa nchi mbalimbali huzitumia pindi wanapofika nchini. Hoteli hizo zilizoko katikati ya jiji zimechukuliwa kuanzia Juni Mosi hadi Julai 5.
Uchunguzi huo umebaini kuwa,wageni waliochukua nafasi katika hoteli hizo wataanza kufika kati ya Juni 25 na kuondoka Julai 5.
Mpaka sasa hali ya usalama katika hoteli hizo umeimarishwa ili kuhakikisha kuwa wateja wanaowasili katika maeneo hayo wanaishi katika mazingira salama.
Mwananchi

2 comments:

Anonymous said...

sipati picha wataqni wetu wa jadi sasa wanajisikiaje na jinsi wanavyotambaga huyo obama sasa amewaibisha mchana kweupe ya kuwa huyo ni mmarekani tu mnamtambia bure kweli mpende akupendaye ndio mkome kumtambia kila leo watu hawajwi maji kisa mnajivunia mtu ambaye hata hajui kama kuna nchi inaitwa kenya hilooo limewashuka iabu

Anonymous said...

Oh Lord, mpaka Obama aje ndiyo tuongelee jinsi ya kutatua tatizo la umeme Afrika? Are you serious?

Obama has nothing to do with tatizo la umeme Africa. Kenya, Uganda, Rwanda and many African countries have no tatizo la umeme.

This portrays leadership failure and poverty of ambition.