ANGALIA LIVE NEWS
Friday, May 31, 2013
RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AZUNGUMZA NA WANAFUNZI MJINI NANJING JIMBO LA JIANGSU CHINA
Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Elimu za Juu katika Vyuo Vikuu katika Mji wa Nanjing Jimbo la Jiangsu nchini China,wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Sofitel Luxury Hotel,katika mazungumzo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Elimu za Juu katika Vyuo Vikuu katika Mji wa Nanjing Jimbo la Jiangsu nchini China,wakisikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) wakati alipozungumza nao leo katika ukumbi wa mikutano wa Sofitel Luxury Hotel, Mjini Nanjing katika jimbo la Jiangsu akiwa katika ziara ya Kiserikali. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) akiwa na Mama Mwanamwema Shein,kushoto pamoja na Mawaziri na Maofisa aliofuatana nao katika ziatra ya Kiserikali nchini China,Rais alipata muda wa kuzungumza na wanafunzi wa Tanzania wanaosoma katika Vyuo Vikuu mbali mbali, na aliwaelezea hali halisi ya Utulivu na Amani Iliyopo nchini Tanzania ambapo aliwataka kuondokana na wasiwasi.Mwanafunzi Sauli Elingarama ,Dkt wa Bianadamu aliokuwa akiuliza swali mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati wa mazungumzo na Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Vyuo Vikuu vya Mji wa Nanjing Nchini China katika jimbo la Jiangsu,Rais yupo China kwa ziara ya kiserikali.Picha na Ramadhan Othman China
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Mh. Raisi. Wazanzibari ni wangapi hapo kwenye hiyo idadi ya Wanafunzi wa Tanzania?. Jionee mambo kwa macho yako.
Post a Comment