Kikosi cha Simba kinatarajia kushuka dimbani leo kuikaribisha timu ya Mgambo Shooting kutoka jijini Tanga katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam lakini kikiwakosa nyota wake watatu, Mrisho Ngassa, Felix Sunzu na Mussa Mude.
Akizungumza na NIPASHE jana, kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' alisema kuwa wachezaji hao wanapumzishwa kutokana na kuwa na kadi za njano na hiyo ni maalum ili kuwaepushia wasipate kadi nyingine ambazo zitawanyima nafasi ya kuikabili Yanga kwenye mechi ya funga dimba la ligi hiyo itakayofanyika Mei 18.
Julio alisema pia Ngassa mbali na kadi hiyo ya njano pia mshambuliaji huyo wa zamani wa Kagera Sugar, Yanga na Azam anasumbuliwa na malaria.
"Wachezaji wako vizuri na wamefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya kuikabili Mgambo, ila Ngassa ndiyo anasumbuliwa na malaria hivyo alipumzika," alisema kocha huyo.
Aliongeza kwamba Simba inaendelea kujipanga kuhakikisha inashinda mchezo huo na kuongeza kasi ya kuwavaa watani zao Yanga ambao tayari walishatawazwa kuwa mabingwa wapya wa ligi hiyo.
Mgambo Shooting ambayo wiki iliyopita ilifikisha pointi 26 na kujinasua na hatari ya kushuka daraja msimu huu inahitaji kuweka heshima yake kwenye ligi hiyo baada ya mechi yao iliyopita dhidi ya Yanga kumalizika kwa sare ya 1-1.
Simba sasa iko katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha pointi 42 wakati Azam ni ya pili na ina pointi 48.
Ligi hiyo itaendelea tena Jumamosi kwa Azam iliyorejea kutoka Morocco itakapoikaribisha Mgambo Shooting kwenye Uwanja wake wa Azam Complex, ulioko Mbande jijini.
Pazia la ligi linatarajiwa kufungwa Mei 18 mwaka huu ambapo timu zote 14 zitashuka dimbani.
Kufikia sasa ni African Lyon pekee iliyoshuka daraja wakati hatma za Polisi Morogoro na Toto African zimeshikiliwa na Mgambo ambayo ikipata pointi moja tu katika mechi zake tatu zilizobaki itazishusha mbili hizo.
Timu zilizopanda daraja ni Mbeya City ya Mbeya, Ashanti (Dar es Salaam) na Rhino Rangers ya Tabora.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment