Monday, May 20, 2013

Skylight Band yaanda usiku maalum kwa mashabiki wa Man United kumpongeza Sir Alex Ferguson kwa uongozi uliotukuka

IMG_9111
Model Neema Mbuya akishow love na Mtaalam Sound na dereva wa Skylight Band Ludewa kwenye Bango maalum lenye picha la aliyekuwa Kocha wa timu ya Man United Sir Alex Ferguson ambapo Skylight Band iliandaa usiku maalum wa kumpongeza baada ya kutangaza kustaafu kwa mashabiki wa chama hilo.
IMG_9110
Abby Rasta na Meneja wa Band ya Skylight Aneth Kushaba AK47 wakishow love.
IMG_9120
Mwanadada akibusu picha ya Sir Alex Ferguson kuonyesha mapenzi kwa kocha huyo aliyetangaza kustaafu.
IMG_9123
Mdau mpya wa Skylight Band akishow love kwenye bango maalum la kumshukuru Kocha wa Man United Sir Alex Ferguson baada ya kutangaza kustaafu kwa kuingoza timu hiyo kwa miaka 26 na kuipa makombe 13.
IMG_9125
IMG_9131
Meneja wa Skylight Band ambaye pia ni mwimbaji Aneth Kushaba AK47 akiangusha saini yake kwenye Bango maalum la sherehe ya kumuaga aliyekuwa kocha wa Klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson iliyoandaliwa maalum kwa mashabiki wa timu hiyo jijini Dar.
kwa picha zaidi bofya read more

IMG_9176
IMG_9197
IMG_9199
IMG_9195
Mdau Eric Ndalu naye aliwakilisha.
IMG_9274
Dr. Isack naye alitia saini yake kama shabiki wa chama hilo kubwa lililokuwa likiongozwa na Sir Alex Ferguson.
IMG_9141
Sehemu maalum ya kugawa zawadi kwa mashabiki wa Skylight Band.
IMG_9116
Pichani juu na chini Models wakiwahudumia mashabiki wa timu mbalimbali kwa kuwapa bendera na kuwavisha Rizband hii ilikuwa maalum zaidi kwa mashabiki wa chama kubwa la mashetani wekundu Man United kumtakia kila la kheri Kocha Sir Alex Ferguson baada ya kutangaza rasmi kustaafu ukocha. Juu ni Abby Rasta na chini ni Neema Mbuya.
IMG_9178
IMG_9158
Aneth Kushaba AK 47 akitoa burudani naye ni miongoni Waimbaji bora wa kike wa Band wanaowania Tuzo za Kilimanjaro Music Awards 2013 naye yeye pia anaomba kura wewe Mtanzani ampigie sasa kwa kuandika AM 1 tuma kwenda namba 15345.
IMG_9167
Aneth Kushaba AK47 na Sam Mapenzi wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band.
IMG_9188
Mary Lukas vijana wenzake wakitoa burudani kwa Mashabiki wa Skylight Band....Vijana walipendeza na ubunifu wa aina yake. Mpigie kura Mary Lukas anawania Kili Music Awards 2013 kwenye kategori ya Mwimbaji bora wa kikwe wa Band andika AM4 tuma kwenda namba 15345.
IMG_9207
MAFAHARI WAWILI HAWAKAI ZIZI MOJA....Lakini hawa wameweza....Mdau Chiddo (kulia) akiwa na marafiki zake huku wakiwa wameshikilia bendera za timu wazipendazo katika usiku maalum ambao ulikuwa kimichezo zaidi kwa mashabiki wa Skylight Band.
IMG_9353
Wadau wetu wa Ukweli all the way from New Palm Tree Hotel iliyopo Bagamoyo karibu na Hoteli ya Oceanic iliyoungua Mr & Mrs Braiton Robert (kushoto) wakiwa na mdau anayefahamika kwa jina la Pacha (kulia). Wadau mnakaribishwa kutembelea hoteli hiyo Bagamoyo.
IMG_9245
Mbwembwe za mashabiki wa Skylight Band zilianzia hapo.
IMG_9253
Hapo sasa tenwe kazi.....
IMG_9259
Nderemo na vifijo vililipuka katika ukumbi wa Thai Village.
IMG_9264
Sam Mapenzi wa Skylight Band akiimba wimbo maalum wa mashabiki wa timu ya Man United.
IMG_9292
Asiyekuwa na Mwana aeleke jiwe.....
IMG_9295
Burudani ya Skylight Band ikiendelea ndani ya ukumbi wa Thai Village.
IMG_9297
Warembo wakisakata muziki wa Skylight Band.
IMG_9301
Ebwana Camera hii hapa unatumulika mwanangu cheki basi....Jamaa hana hili wala lile mzuka wa kucheza umemkolea kinoma.....
IMG_9302
Sam Mapenzi wa Skylight Band akicheza na shabiki wake.
IMG_9305
Totoz za ukweli zikiendelea kupagawishwa na uimbaji wa Sam Mapenzi.
IMG_9311
Kila mrembo alitaka kucheza na Sam Mapenzi, kijana machachari asali ya warembo.
IMG_9316
IMG_9332
Asali ya warembo Sam Mapenzi akiendelea kupagawisha mashabiki wa Skylight Band.
IMG_9351
Joniko Flower wa Skylight Band naye ni balaa....cheki wadada wanavyopagawa naye.
IMG_9315
Nyomi ya kumwaga si mchezo...Ni Band inayokuja kwa kasi na kukubalika na watu wa rika zote hapa mujini.
IMG_9328
Burudani mwanzo mwisho na watu wastaarabu ndani ya Thai Village.
IMG_9342
Joniko Flower wa Skylight Band akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band.... Anaomba kura yako kama Rapa Bora wa Bendi na Mtunzi Bora wa Mashairi kwenye Kili Tanzania Music Awards tuma neno BG4 au AX3 kwenda namba 15345.
IMG_9355
Shabiki nambari moja wa Skylight Band akijimwaga na sebene lililokuwa likiporomoshwa na Band hiyo.
IMG_9361
Umati wa mashabiki wa Slylight Band ukicheza muziki wa Pwani mduara uliokuwa ukiimbwa na Mary Lukas.
IMG_9365
Usipime wewe Skylight Band ni balaa.
IMG_9372
Mdau Abubakary Abdul na Jembe lake.
IMG_9378
Hemedy a.k.a PHD na Gelly wa Rhymes (kulia) na mdau wakishow love ndani ya Thai Village na Skylight Band.
IMG_9407
Mdau Jacob akishow love.
IMG_9396
IMG_9401  

No comments: