Timu ya Uturuki
Timu ya Uturuki iliyoiifunga Timu ya Tanzania DMV 3-1 magoli yaliyofungwa kipindi cha pili. Timu zote zilienda mapumziko zikiwa 0-0 kipindi cha pili kilianza kwa timu ya Uturuki kuliandama goli la Tanzania DMV mfululizo na hatimae juhudi zao kuzaa matunda kunako dkk ya 62 bao lililopatikana kutokana na mpira wa kona. Baada ya bao hilo timu ya Tanzania DMV ilizinduka usingizini na kulishambulia goli la upinzani kama mbogo aliyejeruhiwa na juhudi kuzaa matundaa dkk ya 67 baada ya Dedi Luba kusawazisha makosa yake kwa kuiandikia Tanzania DMV goli la kusawazisha. Iliwachukua dkk 3 kwa timu ya Uturuki kupata bao la 2 kutokana na makosa ya mabeki wa Tanzania DMV kujisahau. Kunako ddk ya 78 Tanzania DMV ilipata bao la kusawazisha lakini refa alilikataa bao hilo kwa madai mfungaji alikua ameotea. Uturuki walipigilia msumari wa mwisho zikiwa zimebaki ddk 5 mpira kuisha. Hadithi ilikua ile, ubutu wa washambuliaji wa Tanzania DMV ndio uliowagharimu wasiibuke na ushindi leo, walipata nafasi za wazi lakini umaliziaji ulikua mbovu.
Timu ya Tanzania DMV.
Dedi Luba (jezi nyeupe) wa Tanzania DMV aliyefunga goli pekee akijaribu kuumiliki mpira.
Wachezaji wa Uturuki wakijaribu kuokoa hatari iliyokua ikielekea golini kwao.
Wachezaji Seif (9) akisaidiwa na Dullah wakijaribu kumkabili mchezaji wa Uturuki(18)
Captain wa timu ya Tanzania DMV Libe akitikisa bao la pili ambalo refa alilikataa bao hilo.
Wachezaji wa Tanzania DMV wakiokoa mpira wa kona.
Washabiki na wachezaji wakifuatilia mpambano. Raisi wa Tanzania DMV, Iddy Sandaly,(kushoto), Dedi, na Manyoka.
James na Seif walivyopumzika kipindi cha pili.
Mchezaji wa Uturuki (Turkey) akitikisa goli la tatu kutokea mpira wa kona.
2 comments:
Mmejitahiji!!!.Ongeza ufanisi, busara na jitiada mapema kwa mechi zijazo.Hakuna kufa moyo. Ingia gym piza zoezi. Tukakuwa sawa tuu one day Tanzania Team(Diaspora USA)
Asanteni kwa kutuwakilisha!!
ASIYE KUBARI KUFUNGWA SI MSHINDANI TUNA SHUKURU SANA KUITANGAZA TANZANIA ? WATANZANIA TUISHIO DMV TUJITOKEZE TUWEZE KUISAIDIA TEAM TANZANIA NI YETU TUIKUBALI TUIPENDE
Post a Comment