ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 5, 2013

TASWIRA MBALIMBALI ZA MLIPUKO ARUSHA MAPEMA LEO

Hali ya eneo mlipuko ulipotokea
Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea
Ulinzi umeimarishwa

Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia. Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi.
Kwa picha zaidi bofya read more

Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
Wanasualama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio
Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh gaundence Lyimo akielekea eneo la tukio kwa miguu baada ya utaratibu wa kutumia magari kuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya watu na magari yaliyoziba njia.
Magesa Mulongo akiteta na RCO wa Mkoa wa Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na wananchi kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa. Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri wa Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo.

4 comments:

Anonymous said...

Watashindwa tuu hao wanatapata na mabomu,u cant win peoples suport by force!!you're -ve in all aspect and u have nothing good to be followed.Hata ukiua huwezi ishi milele na ukifa ndio utajua Mungu wa kweli ni yupi .......Kila goti litapigwa...wap utajua mwenyewe ..think and act

Anonymous said...

SERIKALI INATOA TAMKO GANI MBONA KLA SIKU MAJANGA KANISANI TU KWANI HATUSIKII MAHALA PENGINE YULE PADRI KAUWA MWINGINE KAPIGWA RISASI TENA WOTE NI KATIKA MAENEO YA KANISA AMBAPO WATU WAMEENDA KUABUDU NA SI KULEWA IWEJE HILI KILA SIKU WAKRISTU FUMBUENI MACHO HALI MPAKA LINI

Anonymous said...

kwa kweli this is too much, matukio haya mpaka lini jamani! kama serikali itaendelea kufumbia macho matukio kama haya ipo siku hata wao watashindwa kuishi nchi hii.

Anonymous said...

NADHANI KUNA HAJA YA SERIKALI KUWEKA ULINZI KATIKA MAKANISA YOTE SIKU ZA IBADA VINGINEVYO WIMBO WA AMANI TUNAOUIMBA KILA SIKU UKO MBIONI KUTOWEKA.