Kuna wakati nilifafanua maana ya mapenzi kwa kirefu sana. Ngoja niwakumbushe kidogo, mapenzi ni hisia za ndani kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine, hisia hizi ili ziwe sahihi ni lazima zigongane ndipo neno upendo huanzia hapo.
Kwa maneno mengine, wawili hawa lazima wote wawe na hisia sawa ndipo wapendane. Tunapokuja kwenye mapenzi sasa, inawapasa watu hawa wawe wa jinsia tofauti – mwanamke na mwanaume. Muunganiko wa wapenzi hawa hulenga kujenga maisha ya pamoja. Upo hapo rafiki yangu?
Yes! Mapenzi ni maisha. Kwa hakika maisha yetu hayawezi kukamilika bila kuwepo mapenzi. Ninapozungumza juu ya mapenzi namaanisha yale yanayotoka moyoni kabisa. Si maigizo.
Ikiwa upo katika uhusiano na mpenzi ambaye hakupendi, yaani wewe peke yako ndiyo unayempenda, wewe ni mtumwa wa mapenzi. Kama ndivyo, kwa nini uwe mtumwa?
Unadhani hakuna mwingine ambaye anaweza kukupenda kwa mapenzi ya dhati na penzi hilo likawa kwa pande zote? Inawezekana, huna sababu ya kulazimisha penzi kwa mtu ambaye hakupendi!
Mapenzi ni nguzo ya maisha yetu, kama ukifanikiwa kumpata mpenzi ambaye atakupenda na wewe ukampenda ni wazi kuwa maisha yako yatakuwa yenye furaha na hakika utafurahia maisha yako na huyo mwandani wako. Mapenzi yapo hivyo na kama ukijaribu kuyabadilisha utaumia mwenyewe!
Wakati mwingine unaweza ukapendwa na mpenzi ambaye hujampenda, unadhani kuna ulazima wa wewe kulazimisha kumpenda? Moyo wako umeshazungumza na wewe, umekuweka wazi kuwa hauna mapenzi ya dhati kwa mtu huyo, kwa nini ujilazimishe? Tatizo hili mara nyingi huwa kwa wanawake zaidi!
Anatokea mwanaume anampenda sana, anapomtongoza anajikuta kuwa hampendi, anachokifanya ni kumwambia kuwa atamjibu baadaye! Lengo la kumwambia hivyo ni kwa ajili ya kujipanga na kufikiria! Mapenzi hayafikiriwi ndugu zangu!
Kama mtu unampenda, unapomuona tu siku ya kwanza, moyo wako hutetemeka juu yake na hutamani uambiwe kitu fulani na huyo aliyeuteka moyo wako ghafla. Hii inamaana kuwa atakapokuambia kuwa anakupenda, huwezi kusubiri zaidi, hutakuwa na kitu cha kusubiri, ni nafasi uliyokuwa ukiisubiria kwa hamu sana, na lazima utamkaribisha!
Wiki ijayo tutaendelea, USIKOSE!
No comments:
Post a Comment