Thursday, May 23, 2013

WAZAZI KUKWEPA MAJUKUMU YAO SABABU ZA WATOTO KUJIAJIRI JIJINI MBEYA

Kutoka kushoto ni Fredrick Simon (12), Lushindiho Simkonda (10) na Colyns John (8) wakiwa na mzigo wa tofali

Mtoto Colyns John mwenye umri wa miaka 8 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Ikuti jijini Mbeya (kushoto), akiwa na mwenzake Lushindiho Simkonda (10) ambaye hasomi shule wakiwa wamebeba matofali kuyapeleka walipoajiriwa ambapo kwa kila tofali moja hulipwa shilingi 30.
Anna Simon (8) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ikuti darasa la tatu akiwa amebeba tofali.

Anna na Colyns wakiwa wamebeba mzigo miguuni wakiwa peku majira ya saa 7 mchana ambapo wenzao wanakuwa darasani.

Fredrick (kushoto) akimsihi Colyns asilie maana anakaribia kufika.

PICHA KWA HISANI YA MBEYA YETU BLOG

2 comments:

Anonymous said...

Nimeshindwa kujizuia kulia. Na basi sina neno - Mungu awaongezee neema watawala wa Bongoland!!!!!

Anonymous said...

Wakulaumiwa nani?