Wednesday, May 1, 2013

WOSIA WANGU KAMA IKITOKEA NIMETANGULIA KUFA KABLA YA RUGE AU JOE KUSAGA

Mwanamuziki Lady Jay Dee
Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesiNa bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.

Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.

Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.

Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.

Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.

Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.

Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao. Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.

Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige mawe
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.

Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.

Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.

Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia, kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..

Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.

Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani?? Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??

Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.

Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??

Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu

JIDE

11 comments:

Anonymous said...

Naina dada umevumilia siku nyingi hadi ukaamua kutoa joho lako.Nakushuluru sana kwa ukakamavu wako na pia kusimama imara na msimammo wako na pia kujivunia ubora wako.Wasanii wengi hawawezi kufanya ulichofanya kwa kuogopa kupigwa chini au kuumbuliwa na hawa watu wenye pesa ambazo hawatosheki nazo.Mungu ni mkubwa atakulinda lakini pia kuwa mwanagalifu na sehehmu unazokwenda hakikisha una watu ili uisije kupata kibano kutoka kwa vishere wao.Ninakuombea kwa Mungu na wewe jiombe, hakuna litakaloshindikana kwake.Endelea kutupa burudani bila ya woga.weka nyimbo zako kwenye Yutube, itune, na blogs zitasikilizwa dunia nzima hizo redioa zako zinasikilizwa na hapa nyumbani tu.Pole na hongera kwa kusimama imara.

Anonymous said...

Pole sana. Ila nakushauri wasamehe na move forward bila kupoteza muda. Una sifa nzuri usijiharibie na hao wachache.

Anonymous said...

Tuko nyuma yako Dada... Jay Z alipoachana na Damon Dash maneno yalikuwa hayohayo... I made you!!! Jay akajibu katengeneze mwengine kama mimi!! Leo hii Dash yuko wapi? Siku zote watu kama Ruge na Kusaga hawataisha wao wanafikiri ukimuinua msanii basi abaki kukutumikia milele: ( Utashinda tu! Hata hivyo visenti vyao ni vyakunyonya wasanii wakibongo... wewe unakula jasho lako ..uzuri uko juu ya ubaya daima. Much love.

Anonymous said...

Wewe mwanamke una matatizo mimi sina roho mbaya tumekusaidia sana kufika hapo ulipo lakini huna Shukrani wewe ni mchawi una tafuta umaalufu wa bule kupitia kwetu. Clouds does not need your money we have a lot of artists tena wazuri kuliko wewe tuna fanya nao kazi na wanatupenda. Ugomvi wetu sisi na wewe siyo kujitoa au kuamua kufanya kazi mwenyewe kama hatu kupendi ungetuomba pesa tukakupa? Tume kukopa hela nyingi umeweza kununua vifaa vya muziki umeweza kuanzisha hako kahotel sasa leo unaweza kututusi mimi kusaga na Ruge? Kumbuka siku ya kwanza ulipo kuja hukuwa na kitu tuka kusaidia wewe na mume wako pesa ya kwenda china nani alikupa? Tatizo lako una kiburi na kupenda kujifanya mjuaji wakati hujui chochote. Nasema umewataja wafanya bishara wenzangu kusaga na Ruge unasema unanisamehe? Nitaje mimi nina siri nyingi sana za kwako na hata picha za golden tulip ninazo sasa ukizidi kuongea nazitoa. Nani ana shida ya kupiga mziki wako mbovu ukifa? Kuna miziki mingi tu. Narudia ukipenda nitaje mimi siogopi nina habari zako nyingi sana nitaziuza mitaani.

Anonymous said...

Pole sana Lady Jay Dee. Binadamu wengi hawapendi mafanikio ya wenzao, but guess what?
The Lord will open doors that no man can close, and close doors that no man can open! (Rev.3:8).
You are very talented and have a humongous support base both within and outside the country. Continue doing what you do best.
Tunakupenda sana and will always stand by you!

Anonymous said...

Huyo mpambe katumwa na Mabosi wake, kiswahili chenyewe hakijui,inaonye hana akili , sasa picha za Jay Dee na hii issue wapi na wapi, we are talkin about udhulumati wa hao mabosi wako, not siri za Jay Dee, wether mlimkopa or not ..its is a give a take..she had talent thats why u were willing to invest on her, kama sio hivyo msingetaka kumsaidia.
Ila kumsaidia mtu sio ndio mnataka kumuOWN hapana..
your days are numbered wasanii wataamka bongo kama Jay and u will be in big trouble.
Good luck Jidee, we are proud of you

Anonymous said...

Kama kweli unasema ulimsaidia, na wala huna ubaya naye na hauko upande wowote basi jitaje mwenyewe!! Werevu wote wanajua nyinyi na hao watajwa kutumia radio mmenyonya, na bahati ni kuwa wengi maskini na elimu kidogo, but your days are numbered. Meanzisha THT, badala ya kupeleka BASATA imekuwa yenu!! Mmeua chombo cha haki na umoja wa wasanii Tanzania, tunajua hilo. Wasanii Jiungeni achane kuamini hiyo radio na tamasha lao la laki2-5 ndo mafanikio yenu siyo kweli ni unyonaji, mnavipaji vipeni thammani.
Lady JD binti Machozi, waache watoe picha na waseme wamekutoa A-B, hiyo siyo sababu ya Kunyonya watu. just thinking, wapi Sugu, Afande Sele, TMK, Mbdog, etc mbona wapo weng tuu mliowafanyia mbaya!!

Anonymous said...

daah pole sana dada mungu yuko pamoja na ww hao majamaa wadhulumati wakubwa kila mtu anawajua nnachokulaumu ulichelewa kulisema hili,ila ucjali sisi tuko nyuma yako na tutaendelea kusupport music unayofanya na kila chenye mwanzo kina mwisho so ucjali siku za hao jamaa zinahesabika.

Anonymous said...

Binti Machozi!!
na wasanii wote mliolizwa sasa ndo muda wenu wa kujitoa acheni uoga. Clounds FM management tunajua wanachowafanyia wasanii, tuna kumbuka Sugu, Afande Sele, TMK, nk. Kwanini THT isiwe chini ya BASATA? STUDIO ya mixer ya serikali anamiliki nani, nani anafaidi? Kwanini chama cha wasanii chenye usajili halali na wa kudumu BASATA kimepigwa vita?
Wasanii mnathamani sana, tena hamjajua tu, nasikitika kuona mnatoa nyimbo mnatoa hela eti zipigwe, la hasha hiyo siyo sawa, Mkiweza wapigine fullstop kupiga nyimbo zenu muone kama kuna radio ita survive!!!
Lady JD, vita hii ni kubwa, huna fedha wala ushawishi, ila hilo usijali..... silaha yako ni kubwa kuliko hizo....... ni hazina ya wapenda haki, hatutapenda kuona talented guys are living in poor meanwhile few are driving RANGE!!

Anonymous said...

I never liked the station anyway. This CLOUDS FM imekua chanzo kikuu cha mmomonyoko wa maadili kwa vijana wengi wanaokua in this generation. Vipindi vyao vingi vinaenda hewani...yaani kuna wakati hua nashika mdomo..how posible mtu anaongea studio for public anatumia lugha zisizo na staha kabisa. Mara nyingi napenda kusikiliza WAPO radio na vipindi kadhaa Radio One. Ila mdogo wangu ye anapenda Clouds.One day nilikua na dogo tunaenda church katikati ya wiki. Baada ya ibada mi nikawa nimechelewa tulikua na kikao kidogo so nikampa dogo funguo akaenda kwe gari akawa ame tune hiyo Clouds yake. Niliporudi nikawasha gari na kuondoka. Yaani walikua wanatangaza XXL ikawa huyu sijui Mchomvu anaongea upuuzi mambo ya ndani kabisa na Fetty..it was real bad na bahati mbaya nilikua nimepakia kwenye gari baadhi ya watumishi wa mungu kanisani. Nilijisikia aibu sana nikazuga na kutoa.
Pole Jide..wasikutishe, I know Clouds pia watapita na maybe Mungu atainua radio nyingine ku take over. mungu akubariki, natamani nikuone nikutie moyo na maneno ya wokovu. Amen

Anonymous said...

pole sana mdogo wangu JIDDE, Unajua sisi watanzania tuna matatizo ya wivu wa kijinga na kipumbavu, huwa hatutaki kuona mtu anapiga hatua ya kimaendeleo, sasa kwa mfano wewe dada wa watu umejitahidi na fani yako umefikia mahali pazuri na unakoelekea ni kuzuri zaidi katika kazi yako ya muziki, wanga wameanza kukuwangia! Jamani Watanzania tupendaneni jamani laah! tumerogwa na nani kwa tabia hii chafu?? MTU ANAKWEA MTI ANAKARIBIA KUFIKA KWENYE TAWI LA JUU MTU MWINGINE MWENYE ROHO MBAYA TU ANAMVUTA KUMSHUSHA CHINI! ndio hawa watu wanachomfanyia dada yetu JD. WEWE UKO JUU TU hata wakitumia hivyo vijicenti vyao kukuporomosha hawataweza! Mwenyezi Mungu Akubariki sana na akupe ujasiri!