wishoni mwa wiki iliyopita AAR imetoa huduma ya bure ya mafunzo kwa wafanyakazi wa nyumbani wa wawafanyakazi wa CRDB .
Programu hii iliandaliwa na kutolewa na idara ya huduma ya washauri wa kampuni ya bima ya Afya ya AAR (AAR Employees Wellness Program) kwa nia ya kusaidia vijana hawa kuweza kujitambua,Kujithamini na kufahamu jinsi ya kumudu majukumu yao kwa vizuri wanayopewa na waajiri wao (wa CRDB),
“Tunawashukuru sana AAR kwa kutoa huduma hii kwa wahudumu wetu wa nyumbani, kwakua vijana hawa ndio wana muda mwingi wa kukaa na nyumba pamoja na malezi ya watoto wetu kwa mda wote tunapokua kazini , natumai mafunzo haya yatakua na faida kwao na sisi pia kuwa na imani hata tuwapo makazini”. Alisema Meneja Mafunzo CRDB Agnes Robert.
Mafunzo haya yalihusika na mambo mengi mbalimbali, baadhi ikiwa ni, kujitambua na kujithamini, heshima uwepo nyumbani, jinsi ya kulea watoto kiuanagalifu na kuwahudumia endapo wapatapo matatizo ya kiafya na mengineyo, vitu muhimu vya kuzingatia ndani ya nyumba ,Vitu visivyopaswa kufatwa.
“Kwakweli leo tumefurai sana kuja hapa CRDB nakupewa mafunzo na kampuni ya AAR , kwanza kabsa tumepanuka kimawazo, mambo mengi tulkua hatuyajui, na mengine hatukua tunadhani yanaumuhimu lakini leo tunashkuru AAR kwa kutusaidia kuyaelewa na pia kujithamini , kujikubali na kupenda kazi zetu alisema mmoja kati ya wafanyakazi wa nyumbani”. Mariam Kayege
Programu hii inategemea kufanyika tena kwa mara nyingine kwenye makao makuu ya CRDB, na hapo baadae pia kwa kampuni na mashirika mengine mbali mbali nchini.

No comments:
Post a Comment