ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 24, 2013

TANZANIA YAPONGEZWA KWA KULINDA HAKI ZA WAKIMBIZI DUNIANI.

IMG_7558
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Wakimbizi Dunia ambapo amesema anaishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani katika kuhakikisha Wakimbizi wanakuwa katika mikono salama ya Serikali ya Tanzania.
Kila tarehe 20 ya mwezi Juni Dunia inatambua uwepo wa mamilioni ya Wakimbizi Duniani katika kuhakikisha wanasaidiwa Ili kuondokana na hali ya Ukimbizi katika nchi za ugenini.
Aliendelea kusisitiza kwamba ni vigumu kuelewa Mazingira hatarishi ambayo mkimbizi anayapata kutokana na mapigano ya kisiasa, kidini au kikabila ambayo inawalazimisha kuhama katika makazi yao na kwenda katika makazi ambayo hawayafahamu, alisema watu wasiokuwa na makazi wanazidi kuongezeka Duniani mpaka 2012 takribani watu Milioni 3 walikuwa hawana makazi hizi ni kengele za uamsho wa Jumuiya ya Kimataifa kuamka na kuchukua hatua.
IMG_7577
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Pereira A. Silima akizungumzia majukumu ya Serikali katika kuwahudumia Wakimbizi kutoka nchi za jirani zenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika siku ya Wakimbizi Duniani jijini Dar es Salaam.
IMG_7542
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bi. Joyce Mends-Cole akitoa nasaha zake ambapo amesema anatambua uwepo wa Shirika la Wakimbizi nchini Tanzania katika kuendeleza kampeni ya 2011 inayozungumzia umuhimu wa mwamko wa matatizo ya wakimbizi Duniani.
"Sisi Umoja wa Mataifa Tanzia tunasaidia kuhamasisha mwamko huo wa uelewa wa matatizo ya Wakimbizi katika Dunia ya utandawazi ili jamii ijue majanga na madhara ya vita katika familia na kaya".
Pia ameongeza kuwa Shirika la Wakimbizi Duniani litaendelea kuelimisha madhara ya vita katika nchi zinazoendelea ili kupunguza ongezeko la watu wasiokuwa na Makazi Duniani.
IMG_7569
Balozi wa Marekani nchini Mh. Alfonso Lenhardt na Balozi mpya wa Tanzania nchini Marekani Mh. Liberata Mulamula wakifuatilia hotuba mbalimbali katika siku ya Wakimbizi Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa Juma.
IMG_7545
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa maadhimisho hayo.
IMG_7547
Pichani Juu na Chini ni Wageni waalikwa na maafisa mbalimbali wa Umoja wa Mataifa nchini wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakijiri wakati wa maadhimisho hayo.
IMG_7603
IMG_7548
IMG_7546

1 comment:

Anonymous said...

Asante sana kwa kuziona jitihada za TANZANIA kusomeka duniani. Nafikiri kwa mtizamo wangu umefikia wakati pia wa taifa letu kuzienzi pia haki za sisi wenyewe wazawa nikiwa na maana waTanzania halisi. Tumeweza kulinda wakimbizi hadi hata kuwekeza nchini, wakati tukiendelea na kutoa vitambulisho vya kitaifa wizara husika isipokuwa makini ukweli tutasajili hata wale maadui zetu ni muhimu kupata rekodi kamilifu za yule anayepata kitambulisho na kama si mtanzania halisi basi ieleweke yuko vipi na ameomba Jesus au la! Mwananchi asipoteze uhai wake kwa hali ya utata au vyombo husika visifanye kazi hadi kuishia kimyakimya. WaTanzania tuendelee kuiombea nchi yetu amani rains.